Nukuu:
Mahojiano ni marefu kidogo kama 38:55 minutes, hivyo faili ni kubwa linaweza kuchukua muda mrefu zaidi ya ilivyozoeleka likifanya buffering.Inategemea na Internet connection yako.
**CHA MSINGI HAPO TUJIFUNZE WASOMI WETU WA TANGANYIKA VS ZANZIBAR, NI KWELI WANATUTAKIA KHERI HAWA?
**MJADALA HUU UNAWEZA KUWA UKO NYUMA KIWAKATI, HUENDA MAADA INAYOZUNGUMZWA IKAWA HAIENDANI TENA NA HALI HALISI.SUALA LA KARUME KUONGEZWA MUDA LIMESHAPITWA NA WAKATI NA HALIPO TENA KWENYE AJENDA ZA SIASA ZA ZANZIBAR.


Baada kusikiliza maoni haya kilichonidhirikiya ni kuona kuwa Watanganyika wawili mmoja akiwa CCM (Ulimwengu) na mmoja akiwa chadema (Baregu) walikuwa wakiyatilia mashaka maridhiano ya Wazanzibari. Aidha Wazanzibari 2 bwana Enzi na Dr. Mbarouk wao walikuwa wakiunga mkono mapatano ya Wazanzibari. Inaonesha dhahir kuwa Tanganyika hawaitakii mema Zanzibar.
Kipindi kilikuwa kizuri kwani tumepata kusikia mengi ambayo hatuyapati kwenye vyombo vya habari vya Tanzania ambayo vingi viko Tanganyika. Hongera DW kwa kutuonyesha mambo
Assallam Allaykum jamiya ….
Mashaallah;WATINDIGA AU WATANGANYIKA;
HATUTAKI TENA KUTAWALIWA NA MYINYI;
Kwanza hao Kina ULIMWAENGU NA BAREGU,na HUYO JAHIIJ WAO NYERERE LAANA TULLAH’
Mlikua na nia mbaya juu ya zanzibar Yetu lakini sasa ALLAH anakufedhesheni na mambo ya zanzibar yanawahusu wazanzibar wenyewe; maana nyinyi ndio mlioyafanya haya yote mpaka leo zanzibar imefika hapa lakini kwa uwezo wa ALLAH Tutapigania nchi yetu mpaka kiama kisimame/HATUTAKI WATINDIGA MUTULAWALE; INSHAALLAH WAZANZIBAR TUSIRUDI NYUMA HAO HAWANA NIA NJEMA NA ZANZIBAR;WAONGO WANAFIKI WEZI NA MADHULUMAJI WAKUBWA WA HAKI ZETU ZANZIBAR; Shukran;
Mvumilivu.
salaam,
Nafikiri hii sauti iliyotiwa leo katika mzalendo haikutendewa haki wala haitendei haki wanachama na wasomaji.Sauti hiyo ni ya zamani, lakini haikusemwa hivyo na kwa hivyo watu wengi watatoa maoni ambayo hayaendi na wakati.Sifikiri kuwa kulikuwa na haja ya kutumiwa lakini kama ni muhimu kutumika basi maelezo hayo ya time frame yangewekwa.
Ally
Nilikuwa na mazungumzo marefu jana na Shk Ramadhan wa DW, na alikuja nayo hiyo CD.Nilitaka copi ikatokea hitilafu ya kibinadaamu sikuipata, lakini Alhamdulillah baada ya kucheza kwa muda mfupi na mitambo ya DW nimeweza kunyofoa mp3 hiyo na kuileta hapa MZALENDO.Imechapwa tena ili watu wapate kujikumbusha jinsi ya nia ya wenzetu wa upande wa pili wanaodai muungano kwa kudumisha Pan-Afrikanism.
Maana ukiisikiliza hayo maoni ya “the so called wasomi (Baregu/Ulimwengu)”.Unapata picha kamili kwanini miafaka yote ilikuwa ikifeli kumbe wana ajenda zao za kuendelea kutushushia majeshi na kutupigia/kutuua na kutufanyia kila aina ya uchafu kwa watu wetu.
Maasalaam,
MTAALAMU MFROASTY NAOMBA UPUNGUZE TABIA YA KUBWABWAJA OVYO SAA NYENGINE. JITAHIDI KUCHAGUA MANENO NA TAARIFA ZA KUZIWEKA WAZI, USIWE NA TABIYA YA KUCHANUA TU OVYO.
“lakini Alhamdulillah baada ya kucheza kwa muda mfupi na mitambo ya DW nimeweza kunyofoa mp3 hiyo na kuileta hapa MZALENDO”.
HAYO MANENO YAKO HAPO NDIO MAANA ZANLINK WAKASEMA UMEHARIBU MITAMBO YA ZEC, JITAHIDI SANA NA UNACHOZUNGUMZA, USIKAE KAMA ULO KUNYWA MAJI YA CHOONI. MTUME ANASEMA TUJIHADHARI SANA NA ULIMI.
WABILLAH TAUFIYQ, RAMADHANI NJEMA.
Sijabwabwaja nimesema ukweli na menye akili zake kufikiria ni vipi utaipata mp3 ilioko kwenye internet site ya DW, hilo ni jambo lisiloweza kuepukika ni jambo la kawaida hakuna uhalifu wowote hapo kama unavyotaka ifahamike.
Tafuta jengine….
Maasalaam,
mrfroasty
mumekwisha watanganyika na kama munachukulia mifano ya mchonga meno. basi na mukumbuke maneno ya karume kwamba koti likitubbana basi tulivuwe maanaake mwisho chumbe.kuna kitu mujuwe kwamba hakuna mzanzibar anaeweza kumuuwa mzanzibar mwenzake hiyyyyyyyyyyoo abadan. kwa hiyo kama znz ni nchi basi tuwacheyeni wenyewe na maamuzi yetu yaani mnaiba paka nchi. kwataarifa yenu 20011 znz tuna dolayetu kamili.mtakoma mara hii.vizabizabizabina
Muungano kwetu Zanzibar imekuwa ni hasara. Hata kama biashara inapo kuwa na hasara unatakiwa uiache. Kwa maana hiyo hauutaki muungano tena tunataka nchi kwanini munakuwa vinganganizi. Muna majangwa kwa majangwa kutoka Dar es salam to mwanza, na mamilioni karibu 25 million. Sisi Wazanzibar walio ndani na nje basi hatufiki Miliioni 2, yanini taabu jamaani kama Nyerere alisema kwamba Zanzibar wakiwa hawataki tena sitowapiga mabomu. Basi hatutaki jamani…..nia zenu sio nzuri kabisa.Hata mke na mume huachana mambo yanapokuwa hayawi. Wameshika kimezungunzwa nini kimezungumzwa nini baina ya Malim Seif na Amani. Kilichozungunzwa ni Uzanzibar na haki zao na Amani kwa Wanzibari. Nyinyi ni waatalamu wa siasa basi hamujakamata mita tu. Wakati umefika wa kupepesha bendera yetu duniani.
Naona hapa hata huyu jenerali Ulimwengu hakuficha aliposema kama “kuna watu wwanafaidika hadia hii leo kutokana na huu muungano” hata mimi naona hajakosea kwani ni watanganyika pekee ndio wanaofaidika na huu muungano lakini sio sisi Wazanzibari.
Hawa watanganyika wote wawili Bergu na Ulimwengu wameonesha kukereka na haya maridhiano yetu, kwani huyu Ulimwengu kashikilia kwamba kilichozungumzwa kati ya rais Karume na Seif Sharif ni siri licha ya kuelezewa ni nini kilizungumzwa katika mazungumzo yale, na kama kilichozungumzwa wao hawakijui basi na waamuulize rais Kikwete kuna nini Zanzibar tarehe 31 julai? maana yeye anajua na hata kule dodoma alidokeza juu ya hili.
InshaAllah Mungu atayanyoosha
Haya wazalendo mumewasikia Watanganyika waliovaa sura ya Tanzania, wanajidai wanaumwa na matengano na michafuko ya zanzibar. Generali Dunia Suali la kunguni amelikwepa.Jamani hata Wazanzibari wakifanya siri nanyi mwataka kuijua hee!.
Mimi naona watanganyika ndio wenye siri juu ya wazanzibari, sasa mambo hadharani. Nawaunga mkono Dr Sharif na Enzi Talib kwa michango yao madhubuti.Shukurani tumetambua juu ya Tanganyika wanavyong’ania Muungano mchafu.
Mimi nahisi Mr Frost hii makala uiondoe, kwani Wazanzibari tunayo yanayotushughulisha kwa sasa, Tujaribuni kwenda mbele, tusirudi nyuma. Tukawa tunajadili amambo yaliopita.
Tuwekeeni Matokeo yanayojiri Nyumbani ndio lamsingi kwasasa.
Mimi nashauri katika kuweka hizi makala ukurasa wa mbele nimuhimu zikawa ni Habari Mpya zinazokwendana na Hali halisi inayoendelea Nyumbani.
Tusijaribu kuwaondoa watu katika Mood ya Kura yamaoni.
@Zinduka,
Kwa kweli huo mjadala personally naupenda kwa vile umeonesha wazi watu ambao wanajiita wasomi na hawakuonesha kama wana nia yoyote njema na Zanzibar.
Hivyo mjadala huu unatusomesha jinsi gani haswa wenzetu mtazamo wao juu ya Zanzibar.Wakati wazanzibari wanadhani Zanzibar ni nchi ilioungana na Tanganyika.Wenzao wa upande wa pili wanahisi kuwa Zanzibar ni sawa na mkoa tuu mwengine wowote, na wanaona ni haki kwa Zanzibar kupotea na kuwa mkoa.
Si watanganyika wengi wanaotazama Zanzibar kama ni nchi na kueka heshima.Hapo ukisikiliza hao jamaa, utaona ni wabinafsi and they are far from being called Political Analysts by professional.Wameonesha ubinafsi wa hali ya juu, ambao unaonesha wazi jinsi wanavyoikandamiza Zanzibar.
Na hili tunapenda lijulikane Zanzibar.Ni majuzi tuu Msekwa katoka alikotoka anadai tumeunganisha nchi kwa udugu….ndugu ndio wanavyofanyiana hivi ????
Hivyo makala iko katika muda muafaka kwa mtazamo wangu…unless otherwise.But anyway normally tunajaribu kuchapa makala mpya, lakini leo ni sunday tunaweza jikumbusha wasomi wetu wale wa kutoka Butiama!
Asalam aleykum
Kadri siku zinavyokwenda hata wale wasojua basi sasa wanajua kwamba huo udugu wa Zanzibar na Tanganyika ni wa kinafiki. Hamu yao kuona wazanzibari waendelee kuwa duni ili wao wamalize kuchukua kila kitu.
Watu hawa wanambinu nyingi, moja ni kuwachukua viongozi wetu na kuwaziba macho hata wengine kufika wao kujivua uzanzibari wake bila ya kujitambua kwa kufadhiliwa serikali ya bara.
Tizama namna watu hawa walivyo na sumu mbaya hata wengine hivi sasa wanaona makala hii haikufaa kuwekwa hapa kwa kisingizio imepitwa na wakati kwani kuna mambo mengine yanayoendelea sasa, hebu tufahamishane hayo yanayoendelea sasa kiini chake ndio hichi kinachozungumzwa hapa.
Vijana tunahitajika kuijua historia yetu, bila ya historia mabadiliko yetu yataongozwa na hawa kina ulimwengu wanaojivutia kila kitu upande wao. Eti wanadai nao wanaumwa kuona kuna machafuko Zanzibar na kufika kuthubutu kusema wakati Tanzania (Tanganyika)inajivunia kutoa hifadhi kwa wakimbizi,Zanzibar inazalisha wakimbizi.
Kwanini ndugu zetu hawa wasije mbio Zanzibar ili tusiingie aibu ya kuzalisha wakimbizi au zanzibar sio Tanzania?
Jambo lakushangaza, msemaji anakiri kushindwa kwa Rais wa Tanzania kuweka sawa hali ya Zanzibar, sasa wazanzibar wanatafuta njia zao anahoja milioni moja kwanini wanataka kufahamiana na kuishi kwa amani.
Huu wakati wa vitendo sio wakati wa maneno, AMKENI vijana msizibwe macho na ULIMWENGU. Tusiwe sisi tu ndio tunaona vibaya kusema na kufanya kweli, tufahamu kuwa kama sisi tunaona vibaya wenzetu hawaoni vibaya na wako tayari kufanya lolote kuhakikisha tunaendelea kuwa “hewallah” kwao daima.
haya mahojiano nishayasikiliza kabla na mie sioni tatizo kuwa yamewekwa tena hususan kwa kipindi hichi kuelekea kura ya maoni ningekuwa na uwezo ningependa wazanzibari wote wakayasikia haya,na naamini yangeleta athari kubwa kuwahamasisha watu kupiga kura ya ndio. haiwezekani haya maridhiano yawatie khofu wao na kutaka kudadisi nini kilichozungumzwa,kama wa kuhoji ni sisi hebu tuwachieni.
mnajua nyie nikwambieni hawa jamaa kama alivyosema ulimwengu kuwa kutokana na maelezo ya enzi talib na dr sharif anapata dalili kuwa moja ya mambo yalozungumzwa itakuwa ni masuala ya muungano na hilo ndo khasa linalokhofiwa.Inshallah allah awe pamoja na sisi lakini jamaa hawa ni hatari mbinu zao wanajua wazi kura ya ndio ndo utakuwa mwisho wa vitimbi vyao, watu wawe makini na huu ndio wakati muafaka laa sihivyo tumeingia kwenye mdomo wa chewa Mungu atuepushe na hilo inshallah.
Uwongozi wa Mzalendo, asalam aleikum.
Ningependa kuuliza kama mtandao wa Mzalendo upo kwenye matengenezo kidogo. sababu ya kuuliza ni kuwa tangu nifunguwe habari ya.
sauti: Zanzibar inaelekea wapi?
habari zote mpya zilizokuwa kichwa cha habari zimepotea zimebaki mbili tu hata niki bofya mwanzo(home)inakuja
1:Mchango wa znz walio nje(wazanje)
2:Zanzibar inaelekea wapi?
naomba niulize ni mimi ama mitambo yenu ya kiufundi ipo kwenye matengenezo.
Hakuna matangenezo yoyote kwa wakati wa matukio muhimu Zanzibar.Tumefanya mabadiliko madogo sana kwenye viungo vya site zengine hapo kwenye sidebar upande wa kulia.Lakini hio haina athari zoztoe kama unazozungumzia hapa.
Kitu ambacho nakijua mimi chapisho lina faili kubwa kidogo, hivyo ukibonyeza play inakawia kidogo na kukaa buffering.Hii haizidi dakika 3-5.
Kama bado unapata matatizo ya kiufundi wasiliana na uongozi admin@mzalendo.net au stonetown@mzalendo.net.
Mf Froasty,
Ni sawa ulivyosema, lakini ufahamu pia Siasa ni umakini pia wakuhakikisha unachotaka unakipata, Kwahio Si kila wakati unaweza kuonyesha hisia zako waziwazi. Huenda ukaharibu na kumfanya Adui ashtuke na kujua unalengo baya kwake.oa nafasi ya Majadiliano ya kututoa katika lengo kuu lililopo.
Sisi sote tunajua wanaopinga kura ya Maoni Zanzibar sasa hivi na kupita chini kwa chini ni wazanzibar, na hao ndio waliokua wakijifanya Janjaweed, sasa Mwisho wao unakaribia ndio ukaona vitimbi vyao.
Nilisema kipindi hichi ni cha kufanya Kura ya maoni inafanikiwa, sio kuonyesha kwamaba sisi tunamatatizo na Bara na kuonyesha hisia mbaya kwao. haya yanaweza kuwatisha na tukitaka tusitake Zanzibar imetawaliwa. sasa kunataka Hekma na Busara na mbinu madhubuti kufikia lengo.
Muono wangu hisia zetu wakati mwengine huwatisha hawa na hata baadhi ya maamuzi ya Wazanzibari kuyakandamiza, kwa hofu zinazotokana na hisia zetu na maneno yetu.
Ukweli tunaujua, tufanyeni kweli kivitendo sio maneno. yanayojiri nyumbani nimiongoni mwa vitendo, tuendelezeni hayo.
Tuchezeni na wakati, baadhi ya wakati tuutumieni kuwaeleza na mwengine tufanyeni vitendo.
Narudia tena mawazo yangu, wakati huu nikukaa na kangalia hali inavyokwenda na kujadili njia zinaoweza kutumiwa kuharibu yanayojiri, sio kujadili hawa hawatupendi hayo tunajaua na tunaendelea kujua kwamba hawatupendi na ni maadui zetu.
sawa zinduka maneno yako nakubaliana na wewe lakini wakati mwengine hisia zinakuja kutokana na uzito wa jambo lenyewe,watu wanapoonesha wanatuonea huruma ilhali wanatafuta njia ya kutumaliza huoni hapo mtu inabidi utumie kila nukta kuwazindua watu na kuwahamasisha ili wasije wakalichukulia mchezo jambo hili.
tunaomba uongozi watutilie ule mkutano wa maalim seif unao sema zanzibar sinchi tukumbushane maneno mazito ya maalim hapa na hali ya sasa zanzibar
ahsanten
@Zinduka,
Nakufahamu kwa upande mmoja na upande mwengine napata harufu za woga kutoka kwenye maoni yako.Zanzibar kunatakiwa mhamasisho wa kugombania uhuru kwa mara ya pili au na ya mwisho inshallah.
Hivyo mie sioni ubaya wowote kwa watu wa upande wa pili kujua kama wazanzibari wamevinjari hawataki muungano.Hili nadhani wanalijua by now, wanajifanya punguani tuu…but time will tell inshallah!
@Muddy,
Sidhani kama mkutano huo DVD yake imetufikia MZALENDO.Kwani tumefungua mtandao wakati tukio hilo la nchi si nchi lishapita…Jaribu kutembelea maktaba ya video za MZALENDO mzalendo.blip.tv