Audio

Sheha wasusiwa Maiti

SHEHA, MAITI WASUSIWA – NUNGWI

Kutoka Nungwi

Wananchi wa maeneo mbali mbali nchini Zanzibar wameendelea na migomo dhidi ya Wafuasi wa ccm pamoja na Serikali ya Dr Shein.

Katika tukio ambalo limetokea hivi karibuni katika kijiji cha Nugwi, wananchi wa eneo hilo walimgomea sheha wa shehia ya Nungwi kiungani KOMBO MKUNI kwa kumwambia kua hawamtambui yeye na Dr shein.

Wananchi hao waliamua kumgomea sheha huyo baada ya kituo cha Huduma za Kisheria (Zanzibar Legal Services) wakiambatana na wageni kutoka nje kwenda kwa wananchi kutoa elimu ya sheria na haki za wananchi.

Katika ziara hiyo, Kituo hicho kiliongozana na sheha huyo alogomewa, na wananchi kuamua kumgomea kwa madai kua hawamtambui na hana uhalali wa kuongoza yeye na serikali yake,

Baada ya mvutano mkubwa, Hatimae sheha aliamua kuondoka na Wageni wa sheria na haki za binaadam wakaanza kutoa elimu kwa wananchi hao,

Wakati huo huo, katika eneo hilo hilo la Nugwi, wananchi katika kuendeleza kile wanachokiita mgomo dhidi ya wafuasi wa ccm, Waliamua kususia maiti ya mwana ccm aliyetambulika kwa jina la Jadi haji Mussa na kujikuta maziko hayo hayana watu zaidi ya watu wake wa familia ya marehem,

Tukumbuke kwamba, muendelezo huu wa migomo umetokana na wananchi kudai kua serikali ya dr shein imebaka maamuzi ya wananchi waliyofanya ktk uchaguzi wa Octoba 2015 baada ya Tume ya uchaguzi kuufuta uchaguzi na matokeo yake.

Chanzo na Mwananchi kutoka Nungwi.

Share: