Habari

Mazungumzo na CCM 2015, maalim Alifeli: ” But Failure is a road to the Greatness”

Asalamu aleikhum Warahamatullah wabarakatuhu ndugu zangu wa Zanzivari wa ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu. Ama sina budi ila kumshukuru Allah SW mwenye wingi wa rehma, na kunipa barka ya afya na uzima ya kuweza kuandika makala hii yenye mada hio hapo juu inayosema. 26.October 2015 maalim Sefu alifeli kutuletea Hakki yetu Wazanzibari.  Hasa pale alipojiingiza katika Mazungumzo na Wahalifu, Madhalimu na Makuhani hawa wa CCM ambao mimi huwafananisha sana na wale Makuhani waliokuwa enzi zile za Mtume Muhammad SAW. Kwani Ndugu Wazanzibari kila Enzi zinakuja na watu wema na Wabaya. Basi Enzi hizi tulizonazo sisi ya 21 Century tuna Makuhani wa CCM.

Nimekuja na makala hii ili kutaka kuwanasihi ndugu zangu Wazanzibari na kuinasihi nafsi yangu kwamba tusichukue Makosa yaliopita na kufanya Maamuzi mabaya ya baadae. Bali Tuchukue Makosa yaliofanywa ( Yaliopita) na iwe ni kigezo chakutuletea matunda mazuri ambayo tulikuwa tunayataka wakati ule uliopita lakini tuliyakosa kwa makosa haya na yale yaliofanywa na viongozi wa Kisiasa ambao tulikuwa tunawategemea. Kuna msemo wa Kizungu unasema hivi. Nanukuu hapo chini

” The road to Athletic Greatness is not Marked by Perfection, but the Ability to Constantly Overcome Advercity and Failure…” Yaani njia ya mwana michezo mzuri, haipimwi kwasababu ya ubora wake; bali ni uwezo na uvimilivu wa matumaini yaliotokana na kufeli kwake”

I therefore would like to say to you my fellow  Zanzibari brothers and sisters , the failure of Maalim Sefu Sharif not bring to “Us”  those   fruits  that we´re once expected;  these would actually be a broad road to our greatness and the´e´e most success. As  one Zanzibari, I am sure Maalim Seif  will use his faluire to bring about a new plan for better 2020.

Maalim hakutuletea kile alichotuahidi katika kipindi chote cha miaka 3½ lakini hakuchoka kudai, nakupambana na mfumo uliokuwepo na naamini makosa yale yamewafanya viongozi wengi wa Upinzani kujiimarisha kistrategic katika uchaguzi ujao 2020. Na hio ndio tunaita Resiliency and Greatness. Kipigo walichokipata  Makuhani wa CCM Tanganyika na Zanzibar October 2015,  nikipigo Kitakatifu cha wale watu waliodhulumiwa. Sasa 2020 watachapwa kipigo kikubwa kuliko hicho na baadhi ya wachapaji watakuwa ni miongoni mwa watu wao  CCM wanaochukizwa na mfumo  mzima wa uongozi wa  Kikuhani unavokwenda.

Musidanganywe na mtu  nawapa mfano huu mdogo kuhusu Mkoloni Mweusi.

Watawala wetu weusi Tanganyika waliokuwa hawajawahi kufika Pemba walikuwa wanadanganywa kwamba Wapemba wabaya, wakorofi. Na hao wanaowapaka Wapemba matope wanawapaka kwa sababu tu ya msimamo wao wa kisiasa dhidi ya chama cha Kikuhani na mfumo wake Kristo. Na watu wengi wa Bara walifikiria hivo walivoambiwa, au walifikiria kwamba Wapemba wote ni matajiri kama wanavo waona wale Wapemba walio Invest Kule Bara. Lakini wengi wao walipopata nafasi yakufika Pemba na kukuona na baadae kukaa na watu wa Pemba. Wameweza kufahamu kwanini Wapemba wamekuwa Wakiinyima CCM Kura kwamiaka zaidi ya 54 sasa. Na wengine wameona jinsi watu wapemba walivo wakarimu na watulivu ambao wamekinai katika nyoyo zao. Na sio kwa Utajiri bali nikumshiba Mungu na kuendelea kusoma  kutokana na makosa yaliotokea katika nyakati za nyuma.

Nimepata uthibitisho wa haya kutoka kwa Watanganyika mbali mbali ambao wame mwagwa  kule Pemba  nakufanya ndio makazi yao tokea kumalizika kwa Uchaguzi wa 2015.  Na wengine ni majeshi wenye rank kubwa kubwa, wanakiri kwamba Wapemba au Wazanzibari kwa ujumla hawatendewi vyema na SMZ au ST. Wanaona angalau kule Bara kumenyanyuka kwa majengo na barabara nzuri  lakini Pemba hakuna improvement yoyote. Na hili ndilo liloifanya Pemba kuwa the Great of Opposition party, wapemba hawahitaji campeni za uchaguzi, wana evaluate matendo ya viongozi wa Kikuhani nakuwachapa kwenye “Balot Paper”.  Wengi wa wafanyakazi wa Kijeshi hawa wakimaliza muda wao wa kazi hu takiwa kurudishwa katika Mikoa yao ya Tanganyika waliotoka au sehemu nyengine za Bara. Cha ajabu wengi wao huhiari kulipa rushwa ili wabakie kuishi Pemba kutokana na amani na ukarimu wanaoupata kwa Wapemba.

Tukirudi kwenye mada nilio ianza hapo juu, nina maana kwamba tuacheni lawama kwanini Maalim Sefu alifanya vile alivofanya 2015. Naamini kwavile alikuwa na ushahidi alijuwa kama haki ingetendeka, lakini alisahau kwamba pale alipokaa na wale wajumbe wa CCM alikua mtu mwenye Dini na anae heshimu Haki ni yeye tu. Wale wengine ni Makuhani ambao wanaweza ku ukyadhibisha  ukweli(kuukataa ukweli).

Kwa upande wa CUF na Maalim Sefu pale walipata mafunzo mengine ya elimu ambayo naamini ndio Njia yakutufikisha kule tunakotaka kwenda by 2020. Musisikie kwamba 2020 Kutakuwa hakuna Upinzani. Labda CUF jina litakuwa halipo lakini Wazanzibari watakuwapo na Zanzibar itaendelea kuwepo hadi mwisho wa Dunia. Ikiwa Zanzibar na Wazanzibari wapo basi CCM haiwezi kushinda Uchaguzi. Kwasababu hata humo ndani ya Jeshi lao kuna wanajeshi wanapingana na Utawala huu wa Kikuhani na wanataka mabadiliko na Utawala bora unao heshimu Katiba ya Nchi na Sheria. Na si vyenginevo.

Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisema kwamba maalim Sefu aliiacha chance yakuipata Zanzibar 28.Oct. 2015. But so what, that was a past and the past will  always remain  as a history- the history should unfold and they should considered a ” Great Sccess” Najuwa history ikiwa haina justice inatuletea  majonzi na simanzi (troumar). Lakini hii ndio itakuwa ni ngao yakutupeleka kule tunakotaka. Tukumbuke History ya Watu wa Europe wakati walipo pigana vita vya kwanza na vya pili vya Dunia. Millions of young people ware  left dead. Lakini iliwapelekea kuheshimiana na kuweza kuunda umoja wa Nchi za Ulaya nakuvichukulia vita vile kama somo lakuwasomesha katika kufikia katika democrasia. Tunaona matunda yake hivi sasa, na sisi haya yaliopita yote yawe ni nguzo yakutuweka pamoja, kutetea haki yetu. Hakika Muislamu anaepigania Nchi yake na kuuondoa Utawala mbovu kwa mikono yake, Ulimi au moyo wake basi anfadhila kubwa mbele ya Allah SW.

Katika kipindi hiki cha miaka 3½ ya Utawala huu wa Kikuhani uliowekwa na Jeshi la Tanganyika, tumeona maadili jinsi gani Wazanzibari walivoathirika mara 100 zaidi na pale tulipokuwa na utawala wa GNU. Sio hivo tuu maadili yetu yamebadilika hata lugha yetu sasa tunaipoteza, unamkuta mtoto wa Kizanzibari anaongea kiswahili kibovu cha kibara. Watoto kubakwa na kunyongwa. watu kupigwa pigwa mapanga, njaa na woga wa mtu kuogopa hata kutetea kile anachoamini kama ni haki yake.   Sisemi kama haya yoote ya ngeondoka kwa kipindi kifupi. Bali tungeanza kuyapunguza maovu kwakufanya reconciliation sisi wenyewe na baadae kuangalia community zetu. Huu ndio utawala mzuri na ndio utawala unafuatwa na Watu wa Scandanevian ambao wanapata tunzo yakuitwa watu Wenye Furaha duniani. kama tungekuwa tumepata uongozi tulio utaka sisi wananchi, tungeweza kusema na kukosoa bila yakutiwa mahabusi ya Tanganyika.  Umoja na ihsani imekufa, misikiti na makanisa yamejaa  waumini woga na wengine wanafiki.

Ukija kwa jirani zetu Tanganyika miaka 3½ imeweza kuwapa mambo mengi ya kijamii na  ile bugudha bugudha tuliokuwa tukiisikia kuhusiana na GNU ya Zanzibar imeodoka. Tuchukulie mfano wa Wakoloni Weusi.

Tunawaona Watanganyika inapokuja suali la Muungano wote huusimama kitu kimoja na kuulinda  muungano wao haramu hali yakuwa wanajuwa kama hautendi haki.  Hii ni kwasababu Muungano Ni Cover yao yakuijenga Nchi yao na kuwa imara. Leo hii mikoa mingi ya Tanganyika imejengwa Viwanja vizuri vya Ndege. Hio yoote ni miradi ya Maendeleo ambayo husimamiwa na Serikali. Kwanini Ikiwa Serikali ya Muungano ndio yenye mamlaka mbona miradi hii hailetwi kule Zanzibar?

Hawa Wapinzani wanaofunguliwa kesi kubwa kubwa na kutekwa au kupigwa risasi, nikwasababu wameungana na Maalim Sefu nakuunda Umoja wa UKAWA. Sasa wamewaona hawa ni Wasaliti ya Mfumo wa Muungano na Ukuhani wa CCM- ndio hao wanao adhibiwa nakuwaona wanafunguliwa kesi hizi na zile. Tumeweza kumsikia Raisi Wa Makuhani akisema, Watu wanaoipinga Serikali ya Kikuhani ni Wahalifu na washuhulikiwe.

Nilichokusudia katika makala yoote nikwamba tusichukue makasa yaliopita ikawa ni kielelezo cha kufanya makosa mengine. Bali iwe ni motivation yakuzaa mbinu mpya ambayo iko effective. Naamini kwamba Dhulma za Makuhani wa CCM  hazitadumu Milele dawamu:

SHAIRI LA ANDAMO: BY M:KH.

 

Hewa imetulizana, kila kitu `metulia

Ndege wanyamazana, viotoni wametua.

Wameshangaa wanyama, hata nao wamepoa

Viumbe vimeduwaa!

 

Mawingu yamefungana, na kijivu yamekuwa.

Yametanda giza pana, nchi nyeusi ´mekuwa.

Pana nvua kubwa sana, punde itainyeshea.

Ndivyo ilivoelekea.

 

Mvua hiyo pana sana, badiliko itatoa.

Ardhi itarowana, rutuba itaitia.

Miti ilolaliana, sasa itajiinua.

neema itaenea.

 

Minyama mikubwa sana, wenzao iloonea.

Sasa haya itaona, kwa neema kuenea.

Magoti itapindana, wadogo kuangukia.

Hakuna wakunamia.

 

Basi jambo la maaana, nikuzidisha madua.

Mvua iwe ya maana, isiwe ya mabalaa.

Miti, kaangukiana, na majumba kubomoa.

wasije Kuijutia.

 

Share: