Habari

26bn/- kutumika ujenzi wa skuli

AUGUST 16, 2018 BY ZANZIBARIYETU

SHILINGI bilioni 26 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi skuli 24, kati ya hizo 14 zitajengwa Unguja na 10 Pemba.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa kitengo cha ununuzi na ugavi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Issa Rashid Hamid, katika hafla ya utiaji saini baina ya wizara hiyo na kampuni za ujenzi.

Alisema ujenzi huo utapunguza tatizo la madarasa Unguja na Pemba ambapo ujezi unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao na kukamilika Septemba mwakani.

Akizitaja kampuni zitakazojenga kuwa ni CRJE East Africa Ltd, Salem Construction Company Ltd, Rans Company Ltd.

Kampuni nyengine ni Badr East Africa Enterprises na Home Africa Investment Corporation Ltd.

Skuli hizo zitajengwa katika maeneo ya Mwanakwerekwe, Jango’mbe, Kisauni, Tumbatu, Mkwajuni, Kijini, Mahonda, Kitope, Chuini, Mtoni Kitomeni, Uroa, Unguja Ukuu, Regezamwendo na Bwejuu kwa Unguja.

Kwa wa Pemba ni Wingwi, Kiuyu, Makangale, Kisiwapanza, Mtambile, Kilindi, Pujini, Kojani, Fundo na Limbani.

Alisema baada ya kumalizika ujenzi wa skuli hizo pia wanatarajia kununua vifaa vya ICT, vifaa vya maabara na na vitabu vya kujifunzia na kufundishia.

Alisema ana imani ujenzi wa skuli hiyo utapunguza mrundikano wa wanafunzi.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Share: