Habari

DR sheni usije kusema zanzibar imepiga hatuwa juu ya sekta ya afya

Asalam alykum wazanzibar wote kwa ujumla leo nimeona niandike hii mada yangu ambayo itazungumzia mambo ya muhimu kwa zanzibar ya sasa kuliko sherehe za mapinduzi

Zanzibar na serekali yake wanasheherkea sherehe za mapinduzi ambazo zinagharimu mamilioni ya shilingi za walipa kodi hali ya kuwa hao walipa kodi wanahitaji mambo muhimu ili waweze kufanya kazi na kulipa hiyo kodi likiwemo afya na elimu

DR sheni akisema Zanzibar imepiga hatuwa katika sekta ya afya hutuba yake huu utakuwa ni uwongo mkubwa wa kuwadanganya wananchi wake ambao ndio walipa kodi wa sherehe za serekali  sababu

1} Zanzibar hospitali kuu watu wanafungwa vidonda wakiwa wodini kiasi ambacho kumevunjwa sheria zate za aceptic na anticeptic  hili limekuja kwa nini?

Sababu hospitali yetu haina hata chumba cha kufungia vidonda dressing room

2}hospitali yetu ya mnazi moja inakosa hata xray za contras ambazo zinaweza kuchunguza maradhi ya maziwa kwa kina mama maradhi ya mishipa ya damu maradhi ya herpato biliar

Hospitali yetu pia inakabiliwa na tatizo la kuzidiwa na idadi ya watu ambao watu wote wa unguja na pemba ndio huitumia hospitali hii eti ndio hospitali kuu , nini kifanyike ili kukabiliana na tatizo hil? Tunaweza tatuwa tatizo hili kama ifuatavyo

1}kujenga hospitali tano zenye uwezo kama mnazi mmoja ikibidi hata kulingana kimajengo kwa kila mkowa wa Zanzibar

Kasha mazi moja inabadilika inakuwa ni chuokikuu cha masomo ya udactari kikiwa chini ya uongozi wa suza, tatizo liko wapi juu ya utekelezaji mpango huu? Jibu

Utaambiwa ya kuwa serekali ya mapinduzi ya Zanzibar haina pesa za kujenga hospitali hizi je ?ni kweli serekali haina pesa?

Jibu kwa nini serekali ya smz ipoteze milioni 700 kwa kusheherekea sherehe za mapinduzi  wakati pesa hizi zinatosha kujenga hospitali moja yenye uwezo kama hositali ya mnazi moja kwa mkowa moja hivyo, smz ikizuiya kusheherekea sherehe za mapinduzi kwa miaka mitano itakuwa imeweza kujenga hospitali hizi tano kutokana na pesa za sherehe

Kwa nini sherehe za mapinduzi zisimalizike kwa wazanzibari kupewa kwa mapumziko ya kazi ya siku moja na Raisi kutowa hutuba kwenye TVZ na kufunguwa miradi ya maendeleo bila ya kupoteza mapesa yote haya

Leo miaka 50 tena ya mapinduzi mtu anaambiwa weka mpira au kanunuwe mpira wa kuweka kitandani tukufunge kidonda na sikidonda bali donda harufuuuuuuuu

Haya basi na tusheherakee na kuimba Abedi nenda oya oya ninakutuma oya oya nenda kaseme oya yoa mapinduzi itashina daima siku iliyofika kwenye ngoma ndio hii tunaicheza

Share: