Habari

Ahukumiwa kutumikia chuo cha mafunzo miaka minne

March 13, 2018

Imeandikwa na Masanja Mabula –Pemba

Mahakama ya mkoa wa Kaskazini Pemba imemhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka minne kijana Bakar Omar Bakar mkaazi wa shumba ya mjini wilaya ya micheweni baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 amepatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 kosa ambalo amelitenda mwaka 2016.

Awali kabla ya kusomewa hukumu , kijana huyo ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwani kosa hilo ni la kwanza , ombi ambalo limepingwa na upande wa mashitaka .

Mapema mwendesha mashtaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka wa serikali Ramadhan Suleiman Ramadhan ameiomba mahakama itoe adhabu kwali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwake na vijana wengine wenye tabia kama hiyo.

Akisoma huku , hakimu wa mahakama hiyo Makame Mshamba Simgeni amesema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hivyo kumuona kwamba mkosa kisheria na hivyo kumuaru atumikie chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kulipa fidia ya shilingi laki tatu kwa muathiriwa.

Pembatoday

Share: