Habari

Akutwa ameshafariki kwa kutumbukizwa kisimani Pemba

October 1, 2018 – by Manager

Imeandikwa na Salmin Juma , Pemba

Taarifa zilizotufikia hivi sasa kuna mtoto aliyejuulikana kwa jina la Laahira Abdalla Othman mwenye umri wa miezi 8 amefariki dunia kwa madai ya kutumbukizwa katika kisima cha maji huko Kiungoni wete kaskazini Pemba.

Kwa mujibu wa sheha wa shehia ya Kiungoni tutaarifu kuwa , mama wa mtoto alikua anafua huku mwanawe huyo akiwapa watoto wamsaidie kumbeba kwakua isingekua kazi rahisi kufua huku kulea mtoto, watoto hao walikwenda nae nje mtoto mwenzao na ghafla alitokea mtu ambae inakisiwa ni mwanamke aliyevalia vazi la baibui na NINJA.

Aliwapokonya mtoto huyo na kukimbia nae baada ya muda mfupi alijitokeza na kisha aliwaita watoto wale waliyokuwa wamembeba mwenzao na kuwataka kwenda kutazama kisimani kuna nini.

Baada ya kufika walimkuta mtoto waliyombeba(laahira) akiwa anaelea ndani ya kisima hicho hapo hapo mwanamke huyo hakuonekana tena hadi muda huu.

Taarifa zilifikishwa nyumbani kwao mtoto na kwa kwa sheha wa shehia na taratibu za mazishi kufanyika.

Tupo mbioni kukukamilishia taarifa hii MUNGU akituwezesha kuikamilisha tutakuwekea yote kwa ujumla hivi sasa tosheka na taarifa hii fupi kama kidokezo.

PembaToday

Share: