Habari

Aliemuingilia mlevu wa akili Pemba, afungwa miaka 6…

Aliemuingilia mlevu wa akili Pemba, afungwa miaka 6…

Imeandikwa na Haji Nassor

KIJANA Omar Hamad Khamis miaka 19, wa Semewani wilaya ya Chakechake, ameanza kutumikia kifungo cha miaka sita (6) chuo cha mafunzo, baada ya kupatikana na hatia ya kumuingilia mtoto wa kike miaka 17, mwenye ulemavu wa akili.

Mahakama ambayo ilisikiliza mashahidi saba, kwenye kesi hiyo ni ile ya Mkoa Chakechake, chini ya hakimu wake, Hussein Makame Hussein akisadiana na Mwendesha Mashitaka kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Ali Haidari.

Baada ya mahakama hiyo kumaliza kazi ya kuwasikiliza mashahidi hao saba, akiwemo muathirika mwenyewe, ndipo Juni 25, ilipoamua kutoa hukumu kwa kumpeleka chuo cha mafunzo miaka sita, na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi 400,000 kwa muathirika.

Hakimu Hussein, kabla ya kumpa hukumu mshitakiwa huyo kwa kosa la kumuingia mlemavu wa akili, alimpa nafasi ya kujitetea, na kuiomba mahakama hiyo, imuachie huru kwa vile hilo ni kosa lake la kwanza.

“Muheshimiwa hakimu naomba radhi kwa kosa hili, hivyo naioma mahakama yako tukufu, inipe msahama maana, hili ni kosa langu la kwanza,”aliomba mahakamani hapo.

Hata hivyo hakimu Hussein, alilipiga na chini ombi hilo, na kumtaka mshitakiwa kutumikia chuo cha mafunzo miaka sita sambamba na kutakiwa kumpilipa muathirika fidia ya shilingi 400,000.

Awali mahakamani hapo, mshitakiwa huyo ambae alikuwa nje kwa dhamana, baada ya kusota rumande, alidaiwa kumuingilia mtoto wa kike miaka 17, ambae ana ulemavu wa akili, shitaka ambalo awali alilikana.

Mwendesha Mashitaka Ali Haidari, alieleza mahakama hiyo kuwa, katika siku na mwezi usiofahamika mwaka jana, mshitakiwa huyo, alimchukua mtoto huyo na kisha kumuingilia akijua kuwa ni mlevu wa akili.

Ambapo kufanya hivyo ni kosa, kinyume na kifunfu cha 133 cha sheria ya Adhabu no 6 ya mwaka 2004 ya Zanzibar, ambapo mshitakiwa huyo, hadi anahukumiwa Julai 25, alipanda mahakamani mara 12.

Ambapo kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha mashitaka huyo, aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kutokana na makosa hayo, kuonekana kuongeza siku hadi siku licha ya juhudi za serikali za kupambana nayo.

Awali mshitakiwa huyo alifikishwa mahamani hapo Machi 14 mwaka huu, akikabiliwa na shitaka hilo, ambapo jumla ya mashahidi saba akiwemo mtoto mwenyewe, mama mzazi, dada yake, polisi mpelelezi na daktari walithibitisha shtaka hilo.

Hili ni kesi ya mwanzo kwa mwaka huu kuwahi kutokea, kwa kosa la kumuingilia mlemavu wa akili na mshitakiwa kupatikana na hatia.

Share: