Habari

Amir wa Uamsho na wenzake waachiwa katika mazingira ya kutatanisha

Jumuiya ya Uamsho
Jumapili, Machi 4, 2018

Kiongozi wa Uamsho, Amir Haji Khamis na wenzake wanne waliotoweka tangu tarehe 9 mwezi uliopita (9/2/18) katika mazingira ya kutatanisha leo (tarehe 4/3/18) wameachiwa katika mazingira yale yale ya kutatanisha na kila mmoja kaonekana katupwa upande wake.

Imeelezwa kuwa wapo salama, Alhamdulillah. Na Amir Haji anawashukuru watu wote kwa dua zao na kuomba kwa sasa waachiwe.

Hata hivyo, Amir huyo wa Jumuiya ya Uamsho, hakusema walipokuwa, anasema itoshe wao kuwa salama, taarifa zaidi baadaye kwamba, walikuwa wapi na katika mazingira gani.

Chanzo: Mitandao ya Kijamii

Tagsslider
Share: