Habari

Aonavyo Mzee Kondo

Mitandao ya kijamii ndio sumu kubwa inayo leta chuki,uhasama na ubaguzi hapa visiwani kwetu kwa mujibu wa kauli ya huyu Salim Msangi na lile bao letu sisi la CCM la sauti ya Kisonge HAKUNA tusi pale wala uchochezi pale kuna riwaya za alfu lela u lela tu na nyimbo tukufu za chama chetu tawala.

Wekeni sheria mnazo taka/weza na kufikiri za mitandao na kadhalika, wekeni jela kila kiumbe asie imba wimbo wa taifa hili la Tanganyoka sisi ni watu wenye akili timamu na hatuwezi kuendeshwa kama mifugo kwa visingizio vya bendera ya kijani au buluu tunahitaji amani yenye misingi ya haki sio amani ya kulazimishana baada ya kupora, nimesema na nina rudia bunduki sio suluhisho la matatizo yetu ni kalamu na hili mnalijua ndio maana mnaweka sheria za kutuziba midomo lini tutaelewana kuwa haki ya mtu haichukuliki utajifariji kwa muda tu utailipa ukitaka usitake.

Uzalendo wa kujipachika ndio msingi wa ubaguzi tulioweka, zamani tulisema kuwa uchumi wa Unguja UMESHIKWA na vijana wa Pemba sasa uzembe, uvivu na upuuzi wetu wenyewe vijana wa unguja ndio iwe barka na ila tuwatupie ndugu zetu. Baadae tukaja na wao wamesha soma sana na wana elimu ya kutosha na nafasi zote za serekalini wanazo wao kwa hiyo hawa vijana wa Pemba sasa tuwafukuze makazini na badala yake tuweke na kusomesha wetu wa Unguja ili waje kuchukua nafasi zao za urithi hata kama sio haki yao. Sasa kama sote vichwa vibovu tutafaulu vipi? Au kama hata sote tuna akili kama hao maadui wetu wa jadi kutoka Pemba kwani sote hatuwezi kulijenga Taifa hili ni lazima alie soma atoke Makunduchi/Fuoni/Wete peke yake. Jamani tumieni akili japo kidogo haya hayataki elimu ya maana huu ndio ninao upigia kelele hapa siku zote ubaguzi tu hauna mizizi wala mashiko laana pengine kwani sipati tafsiri nyingine.

Harusi iwe yetu sote na misiba tushirikiane ndio tutafanikiwa vinginevyo ni kujipalilia makaa ya moto ukiwaka huu hatoki mtu tuna kila mifano Rwanda, Kenya na kwingineko bado tunafikiri nguvu za dola zitatulinda sisi ccm tusidhurike na vifo au vilema na watao uliwa ni wapinzani peke yao sasa nauliza kwani huko huko yaliko tokea maafa haya nguvu za dola ilikuwa mali ya wapinzani? Sasa kwa nini waliodhurikana kuuwawa hawakuwa wapizani watupu? Tusijidanganye na haya majeshi ya kukodi firimbi ikilia na wao wanatafuta pa kujificha sio wa kumdhuru kiswahili nimesha maliza sijui niongee lugha gani kiarabu wala kisukuma sijui watawala msikie kuwa mnatutayarishia mauti kwa hizi nguvu mnazo tumia jaribuni akili siku moja moja muone faida yake.

Umeona wapi anatafutwa mtu afungwe kwa kosa la kujifungia chumbani kwake hamtukani mtu bali anatoa duku duku lake kuhusu utumwa mpya ulioletwa kwetu kwa ridhaa ya vibaraka kwani viongozi walio takiwa na watu wamedhulumiwa na yule au wale wanaoandika matusi na ubaguzi mchana wakuwatukana wenzao wengine viongozi katika bao la sauti ya kisonge kwani kwa adabu nilikulia na na kufundishwa na wazee wangu sisubutu na siwezi kuliita bao la kisenge itakuwa sikufunzika japokuwa stahili yao kwani yanayoandikwa hapo yanakihirisha nyoyo au nafsi za kila mpenda haki, amani na anae chukia ubaguzi.

kuwa mwana ccm au mwana cuf hakukufanyi wewe au mimi kuwa mnyama au karima ni uungwana wa vitendo na utu kwa watu ndio iwe silaha yetu, tunaogopana bure ili hali wa kuwaogopa tunakwenda kuwafuata huko kwao mrima na kushika misahafu na kuapa kuwatumika kama mahayawani katika kuitokomeza zanzibar yetu bila aibu,sasa nasema tutasema hata kama hamtaki kusikia lakini iko siku mtanikumbuka.

Mzeekondo.

Share: