Habari

Asemavyo Mzee Kondo

Na Mzee Kondo

Tanganyika au mkoloni anae tutawala hapa Zanzibar kwa kuwatumia hawa tunaowaita viongozi au magozi, hakufurahishwa na matokeo ya uchaguzi halali uliopita wa oct 25,matokeo yake dunia nzima inayajua ,uchaguzi huwa haufutwi ovyo ovyo lazima kuwe na sababu ya kushindwa, nchi hizi za kiafiriti au “kiafirika”haya ni matukio ya kawaida katika bara hili lililojaa watu wanaopenda madaraka na kujilimbikizia mali sio viongozi kuliko kuwatumikia watu.

Sisi wananchi wanyonge katika nchi hizi hatuna tofauti na wanyama iwe wa porini au wa kufugwa majumbani,kwa sababu haki hatuna wala hatuwezi kuipata mpaka mwenye kumiliki mifugo kama ni kondoo,bata,kuku au mbuzi apende,sisi ni viteweo kama si vitafunio (asusa) vya karamu za harusi au arubaini za misiba isiyokwisha, katika dhiki hizi za uhai wa muda chini ya chama cha siasa kinachoongoza kwa ubaguzi,mauwaji,utekaji,rushwa,chuki na kila aina ya laana inayoendelea hapa visiwani na huko mrima,ndio hiki chama kinaitwa ccm haya hayasitiriki tena chini ya mwenyekiti wetu mpya Magufuli.

Maalim Seif narudi kwako kwa heshima tupu kwani sina sababu ya kukukosea adabu wala Mola asinijaaalie nikaipata,barua kuandika ni wajibu wako nafahamu,nyingi umeandika na tele zitafuata, sidhani kama unatarajia barua hizi kuleta tofauti au kuzaa matunda,wewe unafanya kazi kama mwana diplomasia, mwana siasa uliebobea katika siasa za amani,ustaarabu na kuvumiliana, ndio maana wengine watakuona na kukuita Bwege lakini hao sio viongozi bali ni wezi.

Ninachotaka ukizingatie kwa sasa Maalim ni hiki,huko tunakoelekea nimekwambia mara nyingi kuwa ni lazima ujipange,hiki chama chako cha “CUF KIMESHAFUTIWA USAJILI” tunachosubiri ni tarehe tu,haya pia unayajua japokuwa huwezi kuyanena kwa sasa,ushindi wako wa kila uchaguzi kwa miaka zaidi ya ishirini, ndio uliotufanya sisi ccm tufikie uamuzi wa kukifuta chama chako,wewe umekuwa sio tishio tu, sasa umekuwa TATIZO SUGU, ccm ime tulazimu kuchukua hatua hizi za ziada na kukiuwa chama chako kwa gharama kubwa ya fedha na maisha ya watu.

Maalim Seif kama unavyojua, Pro-pesa Lipumba ni muajiriwa wa ikulu ya Tanganyika,hizi fedha zote mnazo nyan’ganywa huwa anakabidhiwa yeye kama bakhshishi yake kwa kazi yake nzuri sana anayoifanya kwa niaba ya ccm,ile ruzuku amekwisha ilewea siku tele,na hizi millioni 76 na ushee amesha kabidhiwa kwa ajili ya kulistawisha tawi hewa la cuf,kinacho fanyika sasa ni wewe na chama chako kushindwa kuweka hata senti tano katika benki yoyote hapa Tannzania,kwa sababu ikiwa mna wazo la kufungua akaunti mpya katika benki ya watu wa Zanzibar,kwa kuwa Zanzibar ni nchi ya n’gambo, mna hiari yenu balozi Iddi na wezi wenziwe wanazisubiri.

Maalim huu sio mkakati wa muda mrefu,hii ni mipango mipya iliyokuja baada ya ushindi wako wa mara ya mwisho ambao niliutabiria hapa kuwa utakuwa wa aina yake,kwa sababu wachambuzi wa mambo ya kisiasa wengi hapa visiwani ni watu wa kubabaisha tu,hili jambo liko wazi miaka yote hii kila uchaguzi ukifanyika ushindi wako unaongezeka madhubuti, badala ya kupungua,hili ni kwa sababu Wazanzibari kila kukicha wanatanabahi ”thanks to muamsho and other factors which are obvious like povety,diseases and hunger” HAYA YOTE ANALAUMIWA NDUGU MUUNGANO.

Tumefika mahali mtu anausifia muungano hapa visiwani ili alinde ajira yake tu,au inategemea yuko maskani gani au amezungukwa na watu wa aina gani katika mazungumzo hayo,sasa unamtarajia mtu huyu ukimfungia katika chumba cha kupigia kura, atampa kura yake mgombea wa ccm au Magufuli?binafsi sikumpigia kura mgombea yoyote wa ccm, kwa sababu hawa watu kwangu ni wasaliti tu, na hawana moja la maana wanalo lifanya zaidi ya kutuzidishia umasikini, na kuviuza visiwa hivi kwa Tangayika kwa hofu ya kukuogopa wewe Maalim.

Mahakama za kisutu hata siku moja kwa sasa hawatoweza kutenda haki kwako,hizo kesi mlizofungua kama unavyoziona zinapigwa kalenda au dana dana tu, kwa amri za Magufuli kama ilivyo kesi ya masheikh wa uamsho,ushahidi hauto kamilika mpaka pale msajili atakapo kuwa tayari kukifuta chama chako,sasa amua moja, ushinde kesi asubuhi jioni chama kifutwe au chama kifutwe ili uendelee na kesi, kwa kifupi “its a lose- lose situation” huna pa kupenya, hili ndio lengo letu sisi waungwana wa ccm kwa sasa.

Maalim chama cha siasa ni watu sio kiongozi,majengo au jina la chama,tumia muda ulionao sasa vizuri kwa sababu huna muda mrefu na unatakiwa kufanya matayarisho/maamuzi mapema hata kama wakati wa ‘execution’ haujafika, usisubiri sana mpaka ccm waka fanya maamuzi yao ya kukifisidi chama chako, wakati wewe bado hujajua “your next move”ccm tutakuja kujuta na kulia kilio cha mbwa koko, yaani mdomo wazi tena juu, ikiwa utacheza karata zako kama ninavyoziona hapa.

CCM tumekuzowea na tunatarajia utafanya Kosa/makosa kama uliyofanya huko nyuma, likiwemo la kumbembeleza Lipumba na lile la kuwaambia wafuasi wako WASICHOKOZEKE hili ni kosa kubwa sana unaedelea kulitenda, huu sio wakati wa kauli hizi utawaambiaje wafuasi wako wasichokozeke huku wakipita wakitekwa na kuuwawa?

Ina maana waendelee kuuwawa na kutekwa? hivi ndivyo unavyo maanisha unapotoa kauli za aina hii, kwa nini unashindwa hata kuwaambia WAJIHAMI, kujihami sio kosa katika dini wala utu, kwani siwezi kusema katiba hapa hatufuati katiba wala hakuna katiba, ndio maana watu wanatutawala bila idhini yetu.

Watu wasio julikana na polisi au na wazee wao au mazombi wanavamia usiku/ mchana katika nyumba na vyumba vya wazee na watoto wetu wa kike na kiume,wanapiga na kuwatia vilema,wana wavua nguo watoto wa kike,wanapekua nyumba mpaka nguo za ndani za wazee wetu,kisha wanaondoka na baba mwenye nyumba, wewe unawaomba wafuasi wako wasi chokozeke?wao hawana walinzi nje ya vibanda vyao vya makuti au vya bati bovu/debe kama ulivyo wewe katika ghorofa, Maalim amka ni lazima ujitofautishe na watawala wa mabavu,usiuhubiri ubavu wao tu, ukasau mbavu za wafuasi wako, kwa kuwa zako ziko salama.

Nakuombea kheri kwa Mola kila siku.

Share: