Habari

Asiesikia la mkuu huvunjika guu

ndugu zangu kelele zote zinazopigwa na wataalamu na wafwatiliaji wa hali ya mambo yanavyokwenda wanatowa wasia kuregeza kasi ya kushindikiza kura ya maoni katika hali kama hii ya kulazimisha. wakati mambo kadhaa yaliomuhimu kwa maandalizi ya kura hii hayakukamilika.
sasa hatujui wahusika hawa wanapotaka kutupeleka. lakini kwa upeo wa akili za wengi hali inayotukabili inatupeleka pabaya mno.
waswahili wana msemo wao{ maji yakimwagika hayazoleki} jee yatapokuwa maji hayo yameshamwagika nani wa kulaumiwa?
Mbali na haya ya kura ya maoni yakupitisha katiba mtoriro, bali kuna uchaguzi mkuu ambao hauko mbali. wakati wananchi wengi hawakupata haki ya kuandikishwa katika daftari la wapiga kura, kuna wakati wa kuelimishana juu ya katiba yenyewe, kuna kadhia ya kutokupitishwa ndani ya baraza la wawakilishi katiba pendekezwa mpaka dakika hii kinyume na sheria.Tunaposhikilia kuharakisha mambo haya kwa magube tunakusudia nini? Nchi ichafuke tugawane mbao? kwasabau mabo yatakapochafuka na kuharibika yatakayotokea hayatachaguwa huyu nani na yule nani, yatatufika sote !! jee haya ndio tunayoyataka yatokee kuichafuwa nchi kwa mikono yetu wenyewe?
dalili si nzuri kwa yote ambayo yanayoendelea kutokea kila kukicha, mara majambazi na kuibiwa silaha, mara Alqaida, mara polisi kuuwawa na vituo kuhujumiwa, na kadhalika. jee mambo kama haya tunayatazamaje na kuyapimaje huku tunakoelekea?
Sina la kuengeza ila ndugu zangu wa Mzalendo natuyatafakari haya kwa utulivu ili tujuwe namna ya kujihami na balaa la aina hii lisitokee. { asiesikia la mkuu kuvunjika guu}

V99!!

Share: