Habari

ASKARI WA SMZ(MAZOMiBI) WALIOCHINI YA UONGOZI WA BALAHAU SHEIN, JANA USIKU WALIWAVAMIA WANA CUF KWA LENGO LA KUWAUWA HUKO PANGAWE.

Jana majira ya saa 3.30 usiku Askari wa Vikosi vya SMZ (Mazombi) Wakiwa katika gari aina ya Pickup(nyeupe) ilobeba askari wapatao 20 wakiwa na silaha za moto na kienyeji Walivamia Barza ya Wana CUF Taveta huko Pangawe Wilaya ya Magharib “B” Mkowa wa Mjini Magharib Unguja,Barza ambayo imo katika hatuwa za Mwisho za kukamilisha Uzinduzi wake Rasmi (Baraza ya kusini) umaarufu wake kwani Wengi wa Wana Barza hiyo ni Wana CUF Wenye asili ya Kusini Unguja(paje,jambiani,bwejuu, Muyuni.

Muungoni,Makunduchi) Kuwashambulia Wafuasi wa CUF kwa Mapanga,Mikuki,Nondo,Minyororo,Mashoka,Wafuasi hao wa CUF waliovamiwa ghafla Walikuwa katika barza yao halali bila ya kutarajia kama jana yalikuwa yamepangwa Mauaji dhidi yao. Zahma kubwa ilitokea juu ya Kujinusuru na Maisha yao na ikapelekea kuhujumiwa kwa Mwenyekiti wa Baraza Suleiman Vuwai Lobilo (56) Aziz Mhamed Ali,(42) Mbaraka Pandu Makame (40) na Mzee Maulid Abdalla Chawa (72) ambae huyu alikuwa amelala hapo barazani Mazombi walipovamia na Walimpiga vibaya sana na kumuibia simu, na pesa. Baada ya hujuma hizo kufanyika Askari ( mazombi) waliondoka kwa haraka
Tukio hilo limeripotiwa polisi kituo kidogo cha kijito Upele na Majeruhi wa unyama huo kupelekwa hospitali na Wana CUF Wenziwao kwa ajili ya Matibabu
Picha ni Mzee Chawa (72) alie hujumiwa akiwa amelala hapo barazani wakati wa Uvamizi.

Tagsslider
Share: