Habari

ASSASSINS wa LISSU 2: Master mind Makonda, Musiba, Mwingulu

BY James Maponda:

Inaendelea sehemu ya 2

Habari zenu ndugu Watanzania wa ndani na nje ya Nchi yetu. Naendelea na makala yangu ambayo niliwekewa hapa Mzalendo.net siku ya Ijumaa ya talehe 15.Febuary 2019.

Kwanini Mwingulu Nchembe aliondolewa nafasi yake ya Wazili wa Mambo ya Ndani?

Ndugu zangu Watanganyika au kama tunavopenda kujulikana Watanzania, munakumbuka katika kipindi cha kupigwa risasi Mh. Tundu Lissu na kukimbizwa Nairobi. Magufuli offcourse alitalifiwa habari hiyo kama kazi imefanyika. Source yetu inatwambia kwamba, Magufuli alitoa tamko lakusikitisha sana sanapale aliwaaambia akina Ndugai kwamba kama Lissu amekufa naakimbizwe katika kijiji chake na afanyiwe mazishi huko kimya kimya. Na hataki kusikia BUnge linasimamisha vikao vyake. Hayo ndio matamshi ya Raisi wa Watanzania ambe ni Mkatoliki na anajifanya yeye ni Mpenda haki.

Katika kipindi hiki Mwingulu Nchembe akiwa bado ni waziri wa mambo ya ndani alipendekeza kufanywe Uchanguzu ule wa Ki CCM na sio wa Wataalamu kutoka nje ya nchi. Lakini Mwigulu huyo huyo hakujuwa kwamba zile CCTV Camera zilitolewa pale palipofanyika tukio la Assassin. Alipojuwa kwamba CCTV zirishaondoshwa kwa kuficha ividance. Ndipo alipotaka kujuwa ni nani alizipachuwa. Source inatwambia kwamba, kulikuwa na kutofahamiana baina ya Makonda na Mwingulu. Hasa kwa vile Mwingulu alitaka ufanyike uchuguzi wa kuziba watu macho lakini Makonda, Musiba na Magufuli walikataa. Kwasababu walijuwa unapofanya uchunguzi hata kama ni wa juju juu basi kuna mambo mengine ya sili yanaweza kuwa revealed. Hapo ndipo Mwingulu Nchembe alipoondolewa katika nafasi ya Wazili wa Mambo ya ndani na habari ya Tundu Lissu ikafifia fifia hadi sasa ndio badhi ya Mawaziri wa CCM wanakuja kusema hakukuwa na CCTV.

Kwanini TUNDU LISSU aritakiwa AFE ?

Ndugu Watanzania tunajuwa kwamba Mh. Tundu Lissu ni mtu aliebobea kwa Sheria na ni msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani ambae sio tuu alifichuwa madudu Mengi ya Mikataba mibovu ya rasilimali za Watanzania. Bali alikuwa pia akikemea sana sakata hili la Rasimu ya Katiba ya Warioba,  Kashfa ya ESCROW ambao akina WILLIAM NGELEJA Mbunge wa Sengerema walijigawia pesa hizo millioni 40 ambazo waligawaniwa. Pia JAMES RUGEMARIRA, KIBAIJUNKA; CHENGE na hata  baadhi ya Ma Askofu wengi wa Makanisa waligawiwa fedha  hizo za ESCROW. Na katibu wa KIKWETE alipata 1.6 billion- Lakini fedha hizo hawakupatiwa wale Wazanzibari ambao tunawatawala kimabavu na kwa nguvu ya Jeshi pale Zanzibar?

Tuliona jinsi Mh. Tundu Lissu alivipiga kele sana kuhusiana na budget ya 2016-2017 ambayo budget hupitishwa na Wabunge ndani ya Bunge ambao walichaguliwa na wananchi. Lakini Mpango wa maendeleo  wa 2016-2017 ulikuwa wa maajabu na hakuletwa Bungeni kujadiliwa. Mh. Tundu Lissu na  Wapinzani pia walipiga kelele na  hata ku block baadhi ya vitu. Magufuli hapo alianza kuingilia hata Muhimili wa Bunge kwa kuwazuia wasitowe Develepment Plan ya mwaka wa budget ya 2016-17. Hapo ndipo Mh. Tundu Lissu aliona kwamba Mamlaka hayo raisi hana na wabunge hawataweza kupitisha budget au kuijadili bila yakuona mipango ya maendeleo. Wakati huu Bunge lilimchaguwa yule  TULIA JAKCSON ili akae kama interim Speaker. Kipindi hiki Ndicho Magufuli aliivuruga Budget ya 2016-17 na kuliweka bunge Gizani la Tanzania ambalo linawawakilisha wananchi.

Ndugu Watanzania wenzangu kutokana na hayo machache nilio yataja, Magufuli ariwahi kusema kwamba namnukuu … “Ikiwa kuna mtu anataka kuturudisha nyuma wakati sisi tunataka kwenda mbele basi huyo ni aduwi yetu na hafai kuishi….” Kwahivo Mh. Tundu Lissu kwa muono wa wana CCM waliokuwa Wanachota fedha, hawataki transparent governance, critics, Advices waliona Lissu dawa yake ni KIFO. Mungu hakusimama nao sasa wanafanya njama nyengine na kumkingia Magufuli Kifua.

JEE NI NANI ADUI WA TAIFA?

Mh. Tundu LISSU ndie mmoja aliekuwa akipiga kelele kuhusu uteuzi wa Tulia Jakson ambae yeye alikuwa ni mtumishi wa Raisi Ikulu lakini aliletwa Bungeni kuja kulidhibiti Bunge . Na kama sio kelele za viongozi wa opposition basi TULIA angekuwa ndie Mbunge. Lisu  ametowa onyo kwamba utawala wa Magufuli  unaelekea kwenye  KIDICTATOR. Nakuwahi kusema huyu raisi wetu ni Dictator Uchwara. Mh. Tundu kama Mkuu wa mpizani na mwanasheria mkuu wa Tanganyika Law Society pamoja na elimu yake ya sheria aliona kwamba Magufuli anajipa mamlaka makubwa. Siasa chafu za CCM na ukandamizaji kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar 2015. Masuali ya Muungano na Mh. Tundu Lissu kutaka kuona Mkataba wa Muungano pia ni moja ya mambo yaliomkera Magufuli na Genge lake.

Mh. Tundu Lissu pia alisema Serikaliya Muungano inaiba Mabillion ya fedha na watu hawachukuliwi hatuwa yoyote ile wakati wananchi wanakufa njaa na kukosa maji. Wakati wa Mwingulu Nchembe alipokuwa Naibu waziri wa Fedha na kukaimu uwaziri wa Fedha, Billioni 1.2 zilipotea kwa CCM. Alipofanya mahojiano alisema zilikwenda katika kuimarisha maendeleo vijijini. Maendeleo hayo ukiona yanafanywa  unawaona UVCCM wapo mbele. Hivo Magufuli ametumia Critics za Chadema kutoka kwa Mh. Tundu Lissu. Zitto Kabwe na Wapinzani wengine kuanza kusaka wanarushwa.

Chakushangaza ambacho sisi Watanganyika na hata Koloni letu Zanzibar hawakijuwi nikutokuwa na uwazi wa hao waliokamatwa kama ni wala rushwa.

Jee wamechukuliwa hatuwa gani?

Jee kesi zao zinaendelea vipi?

Viongozi waliotumbuliwa kwa kutuhumiwa kama ni wala rushwa  wa mali ya Umma au mali ya Taifa  kwanini kesi zao ziwe ni Siri kubwa?

Ndipo hapo Mh. Tundu Lissu anaposema Magufuli anasema anatumbua watu wala rushwa kwakutaka kujionyesha. Lakini Ukweli ni kwamba Magufuli na UVCCM ambao wengi sasa wamepachikwa kuwa USALAMA wa TAIFA na Wakuu wa Mikoa ndio Wala Rushwa wakubwa.

Please dont mis the next article.

Usikose Kusoma makala yangu nyengine kuhusiana na Mpango wa kumuondoa CAG muislamu ambae anafanya kazi zake vizuri na kumuweka Mkatoliki ambae ataweza kupitisha fedha zakununuwa Wabunge zaidi ya Wapinzani au Kununuwa Kura za Wananchi 2020.. Huu ni Mpango wa Magufuli na Washauri wake wakubwa akina BASHITE.

 

Share: