Habari

Ataefanya vurugu atakiona cha mtema-kuni – Dr.Shein atoa mkwala!

Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewatahadharisha wanaojiandaa kuleta vurugu visiwani humo kwamba wasije kuilaumu Serikali kwa hatua itakazochukua dhidi yao.

Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika Kisiwandui Zanzibar jana, Dk Shein alisema:

“Tutailinda amani kwa gharama zozote na tutamdhibiti yeyote atakayeleta vurugu… niliambiwa kuna watu wanataka kuleta vurugu, nasema walete hizo vurugu kama wana ubavu.”

Alisema CCM itaendelea kutawala Zanzibar licha ya vibaraka wa ndani kutumika kutaka kukiondoa chama hicho madarakani.

“Mtaiona hivihivi CCM ikiendelea kutawala licha ya majaribio ya vibaraka kutaka kuing’oa, kwenye nchi nyingi vibaraka wamefanikiwa kuviondoa vyama vilivyoleta ukombozi lakini kwa Zanzibar mtaiona hivihivi,” alisema.

Aliwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi wa marudio Machi 20.

Tagsslider
Share: