Habari

Athari za Magufuli kuzuia Watanganyika Kusafiria Zanzibar

Athari za kuzuiliwa Watanganyika kusafiria Zanzibar na serikali ya Magufuli.

Miezi kadhaa isiyozidi 6 Serikali ya Muungano ilizuiya makontena ya wafanyabiashara kutokea Kenya kuingia Zanzibar,hayo hayakutosha wakazuia meli kusajiliwa Zanziba na sasa Abiria kuzuiliwa kurukia Zanzibar,tumeangalia athari kwa ufupi ,licha ya kwamba wanaojidai SMZ kulifumbia macho hili kama mshirika wa Muungano lakini athari zake ni kubwa kuliko unavozifikiria kama zifuatavyo:-

1.Ndege za abiria na Mizigo kuhamishia huduma zao Airport nyengine za karibu kutokana na uchache wa abiria/au abiria wale wale kuanzia safari zao kwengine.

2.Kukoseshwa mapato kwa serikali ya Zanzibar na wadau wengine yanayotokana na Airport mfano tax ya mapato ya Airport (Income Tax) ,Taxi ya abiria,Airlines landing fees,take off fees,parking fees,noise surcharge,emission fees n.k

3.Biashara za karibu ya Airpot kuathirika,mfano mikahawa ,maduka ya kaiwaida ya kitalii n.k.

4.Usafiri kwa ujumla huathirika,mfano Daladala,Taxi usafiri wa majini n.k kutokana abiria
wa Bara huenda ametumia usafiri huo kutoka alipotoka.

5.Mahoteli na nyumba za wageni kukosa kipato kutokana na kukosa abiria hao.

6.Travel agents kukosa kipato kinachotokana na ukatwaji wa ticket za ndege.

7.Biashara ya utalii kuathirika kabisa hasa watalii wa ndani ya nchi.

8.Airport cargo ,customs kukosa kipato ,mfano yanayotokana na mizigo,fines n.k.

9.Huduma kwa mfano za mafuta ya ndege kuathirika kutokana na ndege kutotumia
Airport hiyo na kuhamishia airport nyengine.

10.Kama ndege inatumia local food kwa abiria maana yake ni kukoseshwa kipato kwa
anaefanya chakula cha ndani ya ndege.

11.kubwa zaidi Airport huwa na Fixed income tax ambayo inatakiwa iwe inailipa Serikali,kwa hiyo itakuwa inalipa tax hiyo kwa Serikali bila wao kufikia kiwango hicho kutokana na kuzoofika kwa biashara.

Hizi ni athari kwa ufupi tu lakini Hadi leo serikali inayojiita smz Imekaa kimya wakati Sekta zake za ndani ya nchi zinazowaletea kipato zikiwa zimekatwa mikono kabisa.

Source: (Zanzibar Channel FB)

 

Share: