Habari

Baada ya CUF kususia uchaguzi, nini Mbadala wake?

Leo nimeonelea nije na kijiswali hiki:

“Baada ya CUF kususia uchaguzi, nini Mbadala wake?”

Niwazi fikra za wengi zimeelekea upande mmoja bila ambao ni vyema kususia uchaguzi huu wa Machi 20. Pia wako walioangalia kwa mtazamo mdogo pindi CUF ikiingia kwenye uchaguzi.

Nakumbuka wiki moja kabla ya uchaguzi niliandika makala yenye kuonyesha mapungufu ya kutoitumia kampeni kueleza faida waliyoipata kuwemo kwenye serikali ya umoja kitaifa, wengi waliona kama vile ni usaliti.

Kwa muda nimekuwa nikitafakari juu ya uamuzi mgumu ambao Chama Cha CUF kimeuchukuwa, nao ni uamuzi wa kususia uchaguzi. Bila ya shaka, kwa umaja na maamuzi waliochukuwa walikaa na kutafakari kwa kina, pengine na zaidi ya vile mimi nilivyokaa na kufikiria. Tukumbuke akilini nywele kila mtu ana zake.

Almuhimu nilikuwa nalinganisha faida na hasara za kutishiriiki katika uchaguzi wa Machi 20. Kisha nilitafakari nini mbadala wake utakuwa pindi uamuzi wa upande mmoja utakaposhinda mwengine.

Hivyo basi kabla ya kutoa yale yaliyonijia fikranimwangu, ningependa kwanza niwaachie wazalendo wajifarague kwa mawazo namaoni yao kisha hapo baadae kidogo nitowe yale yakwangu.

Ukumbi ni wenu.

Share: