Habari

Bada ya deal kushtukiziwa Tibaijuka aja na maneno laini lakini ya Ulahai

Waziri wa nyumba na maendeleo ya makaazi Profisa Anna Tibaijuka

TIBAIJUKA AMJIBU JUSSA

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makaazi Profisa Anna Tibaijuka amesema suala ya kugawanya raslimali ndani ya muungano linaweza kujadilika badala ya kuendelea kuzozana juu ya pendekezo la kuomba eneo la maili 200 la bahari kuu ya hindi kwenye umoja wamataifa.

Akizungumza na Zenji Fm radio juu ya mvutano huo ameseema wananchi wanao uhuru wa kujadili raslimali zao kwa kila upande wa muungno na hatimae kupatikana muafaka.

Profisa Tibaijuka amesema wananchi wanaweza kutoa maoni yao juu ya ugawanaji wa raslimali zitakazopatikana katika eneo hilo wakati huu wa kuunda katiba mpaya badala ya kuendelea kubaki chini ya umoja wamataifa.

Aidha Profisa Tibaijuka amesema suala hilo linagusa mipaka ya nchi na limo kwenye mamlaka yake na iwapo eneo hilo litapatikana wizara yake haitakua na mamlaka na raslimali zitakazopatikana ikiwemo nishati ya mafuta.

Hivi karibuni mwakilishi wa jimbo la Mkongwe Ismail Jussa Ladhu ameiomba serikali ya mapinduzi Zanziba kuiandikia serikali ya jamhuri ya muungano kuitaka kusimamisha mpango wake huo wa kuongezewa eneo hilo kwenye umoja wa mataifa.

Akiwasilisha hoja ya dharura katika baraza la wawakilishi amesema suala hilo bado halijapatiwa ufumbuzi kutokana na baraza la wawakilishi kutoa mapendekezo ya eneo la bahari kuu na raslimali zake liwe chini ya mamlaka ya Zanzibar.

Eneo lililombwa na Tanzania kwenye umoja wa mataifa la maili 200 za ziada katika bahari kuu ya Hindi sehemu kubwa liko kaskazini mashariki mwa kisiwa cha Pemba.

Serikali ya jamhuri ya muungano Tanzania imetumia zaidi ya shilingi bilioni moja kama gharama za kuwasilisha pendekezo hilo kwenye umoja wa mataifa huku wajumbe wa baraza la wawakilishi wakidai Zanzibar haikushikishwa kikamilifu.

chanzo islamic news

Share: