Habari

BALOZI SEIF AWATAKA WAISLAM KUFUATA MAFUNDISHO YA MTUME

PEMBA.

JAMII YA KIISLAMU NCHINI IMETAKIWA KUFUATA MAFUNDISHO SAHIHI ALIYOKUWA AKIYASIMAMIA MTUME MUHAMMAD { SAW } ILI KUPATA FURSA NZURI YA KUISHI KATIKA MAISHA YA FURAHA NA USTAARABU WA MAENDELEO MAKUBWA.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ BALOZI SEIF ALI IDDI AMESEMA HAYO KATIKA HAFLA YA MAULIDI YAKUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD { SAW } YALIYOANDALIWA NA CHUO CHA SAMAIL ACADEMY NA KUFANYIKA KATIKA MSIKITI RAHMAN ULIOPO GOMBANI MJINI CHAKE CHAKE KISIWANI NPEMBA.

BALOZI SEIF AMESEMA KUWA KIGEZO CHEMA ALICHOKUWANACHO KIONGOZI HUYO WA WAISLAMU KILIJIKITA ZAIDI KATIKA KUSIMAMIA VYEMA SUALA LA KUDUMISHA AMANI KATIKA DUNIA, KULETA UMOJA BAINA YA WAISLAMU, KUJIKUBALISHA KUISHI NA MAYATIMA SAMBAMBA NA WATU WA RIKA ZOTE BILA YA UBAGUZI.

AIDHA BALOZI SEIF AMEUPONGEZA UONGOZI WA CHUO CHA SAMAIL ACADEMY KWA JUHUDI ZAO WALIZOZICHUKUWA NA HATUA WALIYOIFIKIA KATIKA KUIJENGA JAMII KITAALUMA NA MAADILI YANAYOKUBALIKA.

AKIRIDHIA KUKUBALI KUWA MLEZI WA CHUO HICHO CHA SAMAEL ACADEMY BALOZI SEIF AMEAHIDI KUZISHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU NA WANAFUNZI HAO KWA KUTOA MCHANGO WAKE KULINGANA NA HALI ITAKAVYORUHUSU.

AKISOMA RISALA MUDIRI WA SAMAEIL ACADEMY AL-USTADH SAID ABDULLA NASSOR AMESEMA KUWA TAASISI HIYO ILIYOASISIWA MWAKA 2012 NA KUSAJILIWA RASMI MWAKA 2014 INAJISHUGHULISHA NA MASUALA YA KIJAMII KATIKA MAENEO MBALI MBALI HAPA NCHINI.

MUDIR HUYO AMESEMA KUWA SAMAEL ACADEMY IMEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII KATIKA UCHIMBAJI WA VISIMA, KUUNGANISHA MADRASA KUWA NA NGUVU ZA PAMOJA KUWAKUSANYA WATOTO YATIMA KWA KUWAJENGEA MAZINGIRA BORA YA KIELIMU NA MAISHA YAO YA BAADAE PAMOJA NA KUANZISHA MAFUNZO KWA WALIMU WANAOTOA HOTUBA MISIKITINI.

AKIBAINISHA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWA CHUO HICHO USTADH SAID AMEBAINISHA KUWA NI PAMOJA NA KUZIKUSANYA NA KUZISAJILI MADRASA 95 ZENYE WANAFUNZI ELFU 10,995, KUSAJILI MAYATIMA 712 PAMOJA NA KUZITEMBELEA MADRASA KWA KUANGALIA CHANGAMOTO ZINAZOZIKABILI.

MUDIRI HUYO WA SAMAEL ACADEMY SHEIKH SAID ABDULLA NASSOR AMEFAHAMISHA KWAMBA MOJA KATI YA JAMBO LILILOPEWA KIPAUMBELE NA TAASISI HIYO NI KUWAENDELEZA WANAFUNZI NA VIJANA WALIOFANIKIWA KUMALIZA KUHIFADHI JUZUU 30 ZA QURAN TUKUFU.

HATA HIVYO SHEIKH SAID ALIELEZEA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI TAASISI HIYO KUWA NI PAMOJA NA VIKWAZO KWA BAADHI YA WATENDAJI WA TAASISI ZA UMMA WANAVYOVITOA KWA TAASISI HIYO PAMOJA NA USUMBUFU WA VIFAA VYA MSAADA VINAVYOTOLEWA WANAFADHILI WAKATI WA KUTOLEWA BANDARINI.

AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KATIKA HAFLA HIYO YA MAULIDI YA UZAWA WA MTUME MUHAMMAD { SAW } AFISA MDHAMINI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA PEMBA BWANA OMAR KHAMIS AMESEMA SAMEL ACADEMY TAYARI IMESHAONYESHA NIA SAHIHI YA KUTAKA KUSAIDIA JAMII HAPA NCHINI.

SHEIKH OMAR ALISEMA TAASISI HIYO IKO MBIONI KUJENGA MISIKITI MIKUBWA MITATU KISIWANI PEMBA,MAANDALIZI YA UJENZI WA CHUOKIKUU CHA KIISLAMU CHAMANANGWE PAMOJA NA UJENZI WA CHUO CHA AMALI CHAKE CHAKE PEMBA.

ALISEMA UANZISHWAJI WA CHUO HICHO CHA AMALI UMELENGA KUWAJENGEA MAZINGIRA MAZURI WANAFUNZI WATAKAOPATA TAALUMA KWENYE TAASISI HIYO NA MAANDALIZI YAMEANZA KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA WANAFUNZI HAO WANAPATA AJIRA NDANI NA NJE YA NCHI.

ALIFAFANUA KWAMBA NCHI ZA SAUDI ARABIA NA IRAQ AMBAZO ZIMEAMUWA KUJITOLEA KUSAIDIA HARAKATI ZA UJENZI WA CHUO HICHO CHA AMALI KISIWANI PEMBA ZIMEKUBALI KUWAPOKEA WANAFUNZI WA CHUO HICHO KWA KUWAPATIA FURSA ZA AJIRA KATIKA MATAIFA HAYO.

AKITOA SALAMU ZAKE RAIS WA SAMAEL ACADEMY SHEIKH NASSIR BIN SAID AMESEMA KUWA UONGOZI WA JUMUIYA YA TAASSI HIYO UNAFARAJIKA NA MUITIKIO MKUBWA WA WAZAZI NA WALEZI WALIOOONYESHA KATIKA KUIPOKEA TAASISI HIYO YENYE MNASABA NA MAZINGIRA YAO.

SHEIKH NASSIR AMESEMA KUWA JUHUDI ZITAENDELEA KUCHUKULIWA NA UONGOZI HUO ILI KUONA MALENGO YALIYOKUSUDIWA YA KUSAIDIA JAMII KUKABILIANA NA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUUKA YANAFANIKIWA VYEMA NA KUSTAWISHA JAMII ZAO.

Share: