Habari

BARAZA LA MJI ZANZIBAR (ZMC)

Juzi tumesoma habari kupitia gazeti la Zanzibar Leo/na vyombo vyengine vya habari vya hapa Zanzibar kuwa Baraza la Mji Zanzibar (ZMC) linataka kuzifanya huduma za kusafisha na kuzoa taka ziwe binafsi – privatization.

Inachekesha kidogo kusikia au kuona kjuwa ZMC inashindwa hata kuzoa taka za majumbani ilhali wanakusanya pesa nyini kutokana na huduma hiyo; wanakusanya pesa wanashindwa kutoa huduma – ina maana kuwa wanatapeli watu. Huu ni wizi, utapeli, hadaa na dhulma. Mjini hapa watu wote tumechoka nao maana hawana moja wala mbili.

Pili, kwa nini ZMC waweze kwa ufanisi zaidi kuzitia minyororo gari zilizowekwa sehemu ambazo si za kuegesha magari (within a second) ukiweka vibaya wanakuja wale jamaa [watendaji wa ZMC, wengi wao walikuwa askari wastaafu] kuzitia pingu gari, na in fact, wanazivunja kwa makusudi wakati wanapozibeba.

Vipi ZMZ waweze kutekeleza jukumu lao hili, washindwe kukusanya na kuzoa taka ilhali tunalipia huduma hii, tena kwa pesa nyingi.

Pale maeneo ya Forodhani, wale wanakusanya pesa za parking wanakaa mpaka saa sita — only Zanzibar ndio parking mpaka saa sita usiku. Hili wanaliweza.

Zaidi ya yote — mimi sioni kama ni wazo zuri/muwafaka kuwa huduma kama hii – public utulity kama hii iweze kubinafsishwa – ina hatari athari zake kuliko faida. Tume-privatize banks (service mpak sasa mbovu sana sana, hata ATM hazifanyi kazi most of the times), viwanda – vyote dead n.k kwa ufupi privatization imefanywa kihuni, na inamalizikia kwa wahuni – sio watu w abiashara hasa.

Angalia, baadhi ya halmashauri hapa Zanzibar – wamethubutu kuruhusu kampuni binafsi kufanya kazi kama hii – kuzoa taka. Nyingi zilikuw akampuni kutoka Tanganyika (hayo ndio maradhi yetu); Wallah waliishia kutapeli watu, taka hazikuzolewa, na mbaya zaidi walitumia access hiyo ya kuingia majumbani mwa watu kuiba au kutoa tips kwa wengine na usiku unavamiwa. Hawa makampuni wlaikuwa hwana hata reki au wheel barrow ya kuzolea taka – kweli kampuni hiyo?

Nina wasi wasi kuwa ZMC inalenga kampuni za aina hii kutoka Mrima – Tanganyika ili kutoa huduma ya aina hii. Itakuwa hatari sana kwetu. Hivi kwlei mpaka leo hatujataka kujua, kufahamu kuwa hawa Watanganyika sio watu wazuri kwetu? Mtihani F4 wametufelisha, mafuta wanataka kuyachukua, bahari kuu wanataka kuiiba, mbali dhulma ya BoT, na muungano wenyewe – lipi tena tuonyeshwe na kufahamu jamani. Mbona tumekuwa viziwi sana, vipofu sana, mabubu bubu bubu bubu hata kusema kwa ishara hatuwezi. Msidhani kuwa tutateremshiwa ‘wahyi’ au waje mitume kwa kuttaua matatizo yetu jamani. Ishara zote zipo, Allah anajua kila kitu – ni sisi wenyewe sasa, na yeye atatuongoza.

Jamani amkeniiiiiiii. Msigande na kitanda. Amka….amka.
ZMC waache kudhulumu watu na kutapeli wananchi kw anjia za kuleta vijibarua madukani. Dr.Mwinyihaji Makame Mwadini ndiye waziri in charge wa ZMC – lakini yeye ni mtu aliyejaa scnadals nyingi na zinazohusu hiyo ZMC, na Dr.Shein anajua mengi juu ya haya – na bado amemngangania pale Ikulu. Huyu Dr. mwinyihaji (dr. wa kupiga matuta, ngoro za muhogo – ndio aliyosomea huko Nigeria) hafai – bora arudi Kizimbani agricultural centre.
ZMC wizi mwingi, hadaa nyingi na mji bado mchafu kama walivyo watendaji wenyewe wa ZMC wachafu.

Share: