Habari

Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa

wanabodi.
Amini Usiamini UAMSHO sio UAMSHO tena. yaani Licha ya Vyombo vya habari kuripoti na kupotosha kuhusu UAMSHO. Ndani ya baraza la wawakilishi ni kinyume kabisa, hakuna mwakilishi anaejaribu kulizungumzia, na hata akijaribu kuligusa ni wazi unaweza ukahisi kama analiunga MKono japo sio moja kwa moja.

Katika hali isiyotarajiwa na wengi. Leo hii Wazanibar wametoa madai mazito kuhusu muungano unavyoendeshwa huku Lawama za wazi wazi zikilekezwa kwa Watanganyika kwamba wanawahadaa wazanzibar

Hoja zenyewe:

1) Mh Raza: Ilikuwa ni vigelegele, makofi na hata vicheko vilitanda kila kona barazani huku Spika na Mawaziri wa SMZ wakionekana wazi kupigwa na Butwaa.
Nini Alisema Mh Raza:
No1:
“Mh Spika, nina nyaraka za makubaliano kati ya Serekali ya Awamu ya 3 ya Dk Salmini na Mh Mkapa kuhusu Zanzibar kujiunga OIC. Haya sio maneno ya Mitaani, ninazo nyaraka za makubaliano, na kama serekali ya sasa wanahizaji nitawapa ambazo wenzetu walisema Tanzania itajiunga OIC kwa manufaa ya Zanzibar. Lkn wenzetu wametuhada na wanaendelea kutuhadaa. huku wao wakiwa na UBALOZI wa vertican kwa manufaa yao. Hi ni hadaa kubwa tunayoendelewa kufanyiwa Zanzibar, Hatukubali tena tunasema hatukubali, kwa muungano wa aina hii ” makofi ukumbi mzima.
eti tunaambiwa kupata uanachama wa OIC ni kazi kubwa, naimba serekali hii kazi inepe mimi, ndani ya miezi 3 Tanzania itajiunga na OIC ili tutengezewe madaraja, barabara na vyuo vikuu kama baadhi ya nchi. Zanzibar tunanjaa wao kama Watanzania bara wameshiba waache washibe

No2:
“Mh Spika, niliwahi kusema huko Nyuma, itafika siku vyeti vya ndoa tutakiwa tuvifate Dodoma, nikapuuzwa. sasa unaona, waziri wa nishati wa Tanzania bara leo ndio anawakilisha Wazanzibar ktk jumuia ya Afrika Mashariki huku Waziri huyo akiwa mwisho wake ni CHUMBE tu. hii ni hadaa kubwa tunayohadaiwa wazanzibar huku viongozi wetu wakiwa sio wakweli , sijui nini wanachoogopahili tunasema Tunashachoka, hatulitaki litendeke

No3: Mh spika, miaka 48 ya Muungano hadi kuna watu ndani ya tanganyika wanatuona Zanzibar hatuna maana, leo mawaziri wanakubaliana kutatua tatizo la Muunagno, kuna watu wenye nia mbaya na Zanzibar wanazuia. Muungano kama huu haufai, huu si Muungano, huu ni ulaghai” Makofi.

Mwakilishi wa Kitope
“Mimi naona sasa hakuhitajiki viongozi wasomi kutatua matatizo ya Muungano, tuachaguliwe sisi wasio na Elimu wenye kutoa kauli. maana ndugu zetu hawataki kutusikia.
KWA UFUPI KILA MWAKILISHI INAOENAKANA ANAKWERA NA MUUNGANO HUU UNAVYOENDESHWA licha ya waziri Aboud kudai watu wasubiri katiba mpya. sio CCM SIO CUF

Chanzo: Jamii Forum

Share: