Habari

Bhaa amchana mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi

Mwakilishi wa jimbo la Mtoni, Huseein Ibrahim Makungu (Bhaa) amemtaka mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi kuunda tume maalum kwa ajili ya kumchunguza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud ili kuona anafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar au yake binafsi.

Bhaa ametoa kauli hiyo hayo leo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar wakati akichangia hutba ya makadirio ya mapato ya fedha ya Wizara ya nchi Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ kwa mwaka 2017-2018.

Amesema kuwa utendaji wa Mkuu wa Mkoa huyo bado una mashaka, hivyo yuko tayari kutoa maposho kwa wajumbe wote wa tume hiyo teule ili kufanya uchunguzi huo ambao amesema utasaidia kuona uhalisia wa madaraka ya kiongozi huyo.

Aidha ameongeza kuwa Mkuu huyo amekuwa akifanya kazi kwa kuingilia madaraka yasiomuhusu kwa kupiga marufuku ya kazi kwa baadhi ya wananchi hasa wanaotafuta maisha yao kwa kujiari na kuwaacha wengine wakifanya wanavyotaka.

Bhaa ametoa mfano kwa kusema kuwa Mkuu huyo amepiga marufuku kwa baadhi ya wasanii kufanya shughuli zao hizo, kwa madai kuwa wanasababisha mmong’onyoko wa maadili, huku wengine akiwapa kibali cha kufanya kazi hizo bila ya kuwa na muhali.

Akizungumzia suala la dawa za kulevya Bhaa alisema kuwa pamoja na jitihada zinazofanya na Mkuu huyo katika kupambana na wasika na dawa hizo lakini bado uwazi juu ya suala hilo bado ni kikwazo kikubwa.

Bhaa ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Baraza la Wawalishi amesema kuwa mara nyingi amekuwa anazitaka taarifa za dawa za kulevya ili kumuwezesha kutoa taarifa sahihi katika mkutano wa Bunge lakini Mkuu huyo anashindwa kumpatia ila humjibu zipo tu.

Zanzibardaima

Share: