Habari

Bonanza Pemba

RAFIKI NETWORK KUFANYA BONANZA LA KIHISTORIA KISIWANI PEMBA

 ZURA yalipiga Tafu Bonanza

 AZAM TV Mubashara kutoka Kisiwa cha Marashi ya Karafuu

Na: Ali O. Ali
Kampuni ya Rafiki Network itafanya Tamasha la Michezo na Utamaduni linalojulikana
kama “ Pemba Weekend Bonanza” litakalofanyika kisiwani Pemba kuanzia tarehe 28 hadi
30 Julai mwaka 2017.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa
kampuni hiyo, imesema kwamba “tamasha hilo litajumuisha matukio mbali mbali kama vile
mchezo wa ng’ombe, resi za baiskeli, mashindano ya kuogelea na resi za ngalawa.”

Miongoni mwa matukio, imeelezwa kwamba mchezo wa ng’ombe utafanyika siku ya Ijumaa
tarehe 28 Julai, 2017, majira ya lasiri katika viwanja vya skuli ya Chwale, Wilaya ya Wete,
Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kwamba resi za baiskeli ambazo zitafanyika kwa mizunguko
miwili tafauti zitakuwa siku ya Jumamosi tarehe 29 na Jumapili tarehe 30 Julai katika
maeneo na taratibu tofauti ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa, Siku ya Jumamosi, tarehe 29
Julai, kutakuwa na resi za baiskeli hatua ya mchujo, zitakazofanyika kwa kujumuisha
makundi matatu yanayokimbia kwa kupitia barabara tatu tafauti kiswani Pemba. Fainali za
resi za baisikeli zitaanzia Uwanja wa Gombani hadi Vumawimbi, Makangale Pemba majira
ya saa 1 kamili asubuhi.
Taarifa imethibitisha kuwa kutakuwa na mashindano ya kuogelea baharini yatakayofanyika
siku ya Jumapili, Tarehe 30 Julai 2017 katika fukwe za Vumamwimbi. Shindano hili
litawashirikisha waogeleaji mbalimbali nchini ambapo washiriki wapatao 100 watachuana
katika mpambano huu.

Vile vile taarifa hiyo imesema kwamba kutakuwa na resi za ngalawa zitakazofanyika tarehe
30 Julai, 2017, pia katika fukwe za Vumawimbi Pemba. Shindano litashirikisha ngalawa
takribani 20 kutoka maeneno mbali mbali Kiswaini Pemba kama vile Tumbe, Kiuyu, Msuka,
Shumba Mjini, Mwambe na Mnarani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Tamasha hili limedhaminiwa na ZURA (Zanzibar Utility
Regulatory Authority) na litarushwa hewani na kituo cha Televisheni cha AZAM ambao ni
washirika wenza (Partners) wa Kampuni ya Rafiki Network.

Share: