Habari

BREAKING NEWS: LIPUMBA na UV-CCM kuivamia Mtendeni wakati wowote ule.

Asalamu aleikhum ndugu zangu Wazanzibari wa ndani na nje ya visiwa vyetu adhimu. Nimepata habari muhimu sana na nimeiona ni iweke hapa katika mtandao ili watu wawe tayari kupambana na Uovu huu.  Nimeletewa habari na Source yangu ndani ya CCM, kwamba wametolewa Vijana wa CCM  Kutoka Bara ambao wamepewa Uniform za CUF ili waje kumsaidia Ibrahim Lipumba kuivamia Makao makuu ya CUF Mtendeni.

Mavamizi hayo yana Baraka za SMZ- Sefu Iddi na Haji Omari Heri. Mavamizi hayo yatakuwa yamesimamiwa na baadhi ya Askari kanzu ambao hujiita Usalam wa Taifa au kwa jina la mitaani Zanzibar tunawaita Mazombi au Bara huitwa “Watu Wasiojulikana”.

Kwa upande wangu naona wimbi lakuwakamata Viongozi na Wafuasi wa CUF na kuwaweka ndani Limefikia na baadhi ya Viongozi wa CCM SMZ tayari wana kiu ya Damu za Wazanzibari. Na ndio maana wamepanga uvamizi huu. Hii nitaarifa tuu kuwapatia Wafuasi na viongozi wa CUF. Pengine tayari washapata taarifa hizi.

 

Share: