Habari

Breaking News: Mkutano wa Lipumba leo una baraka za IKULU:

Assaalamu aleikhum warahmatullah wabarakatuh ndugu zamgu Wazanzibari wa ndani na nje ya Visiwa vyetu adhimu. Ama leo hii nataka kuelezea ule usanii nilio ushuhudia katika kile – Polisi wamzuia Lipumba kufanya mkutano  wa MUNGUKI-CUF tarehe 12.March 2019.

Kama tunavojuwa ndugu zangu Wazanzibari kwamba POLISI, MAHAKAMA, MAJAJI na MSAJILI wa VYAMA vya SIASA  au vyombo vya ulinzi na usalama vyengine  viliopo hapa Tanganyika na Zanzibar. Ni vyombo vinavo-tumiliwa na CCM na Serikali yao kufanya mambo MAOVU. Mihimili hii yote imekosa haiba na kuaminika kwa Wananchi wa kawaida na viongozi wa Upinzan,i kwasababu huwa havifanyi HAKI.

Kilicho nistaajabisha leo nikuona kwamba Polisi walikuja kwenye Mkutano wa Lipumba kufanya Usanii na mchezo wa Kuigiza. Na sio ku zuia mkutano wa Lipumba usifanyike. Wiki 2 ziliopita, Lipumba alikatazwa na Mahakama Kuu asifanye mkutano tumepata habari za ndani kwamba.  Kuna “AMRI” imetoka IKULU kwa Raisi kwamba Lipumba aachiwe kufanya mkutano wake kama alivopanga, na Polisi wanalishapangwa kwamba waende pale ili wajifanye kama kwamba wamekuja kuzuia mkutano ule. Na waliamriwa kwamba ikiwa watatokea kundi la CUF watakao mpinga Lipumba washuhulikiwe mara moja.

Ushahidi ni huu tulio uona leo, wakati Polisi walipokuja na magari yao. walikuja kikawaida tu hawana vitambaa vyekundu wala kofia za helmati au Rifal mikononi. Wamekuja pale na walionekana very friendly toward Lipumba au wafuasi wake. Na  Polisi hao walipofika walituniwa kifua na Kijana mmoja Munguki wa Lipumba na Polisi alimwambia kijana calm down.. What?

Polisi afokewe nakutunishiwa kifua na Mpizani na amuache bila ya kummiminia Risasi kifuani kwake au Kuburuza nakumvunja vunja?  Badala yake polisi mmoja alimwambia kijana huyu wa Lipumba” Calm Down” !!! This is something Consperacy. Nakumbuka wakati wa Lipumba alipokuwa CUF kweli na sio Mtumishi wa CCM 2005, Polisi Walimpiga na kumtupa Jela alipofanya maandamano halali. Leo Lipumba ameitisha Mkutano Haramu na alikatazwa kwa barua kwamba asifanye mkutano ule, lakini alikuja nakujifanya anazungumza na simu na kamanda SIRO.. Na kaaondoka bila yakunyukuliwa.

Kama ingekuwa Lipumba ni Mpenzi kweli wa CUF na anaipenda CUF basi leo angeishia Jela. Tumeona Chadema walipokwenda kudai formu za usimamizi wa Uchaguzi mdogo. UKULINA AKULIA Alipigwa risasi za Kifua na kufa hapo hapo, Leo Munguki wa Lipumba anamtanulia kifua Polisi-CCM anaambiwa Calm down… Hii inaonyesha wazi kwamba Lipumba anatumiliwa na CCM na mkutano wake na Polisi ni mipango ilishapangwa na IKULU pamoja na msajili wa vyama (Mutungi). Kinachonichekesha zaidi nikwamba CCM wanaona wata-mfool Maalim Sefu na Watu wake, kumbe wana-jifool wenyewe. Kila ubadhirifu unaofanywa na serikali hii ya CCM na migogoro walioipandikiza ndani ya CUF basi ni Ushaidi mkubwa wakuaminisha kwamba Lipumba anatumiliwa na CCM kwa Maalim Sefu Sharifu na Watu wake,

Kwahabari tulizozipata haswa nikwamba Mkutano huu haukutimia Akidi na kuna baadhi ya watu waliokuja pale ni CCM. Na hii ni mipango ya CCM -Ikulu kuisaidia SMZ kuimaliza CUF Zanzibar. Ujinga ulioje kumuana Mtu mzima ambae ATI amekwenda Makka kukubali kutumiliwa na Mfumo Kristo kuwahujumu  ndugu zake wa kiislamu ambao wamekuwa wakidhulumiwa na mfumo huu miaka nenda miaka rufi. Kila siku najiuliza kwanini CCM Tanganyika na SMZ hawakuchochea ugomvu ndania ya Chadema na kumtumilia Walbraham SLAA? Au tuseme kwamba wameona Cha,ma cha Chadema kinanunulika na CHa CUF hasa upande wa Zanzibar hakinunuliki? Kwanini IKULU na Msajili ajiinvolve direct katika Mkutano huu wa Lipumba?

Hivo Mahakama Kuu iko chini Kuliko IKULU?

Kwanini Serikali ya CCM na Magufuli inawafanya watu wajinga?

Hivo wanadhani kwamba cc tutaamini kwamba polisi wale wamekwenda kutekeleza amri ya mahakama kuu?

Ninachokisema. Wazanzibari tumenyamaza na sio kama tumechoka kudai haki zetu.lakini tunakusanya ushahidi na siku bomu litakapo anguka tutakuwa tuna ushahidi wa Dhuluma sinazofanywa na CCM.

  1. Nawajuwa watu wangu, sababu mimi na wao

Tuna mengi ya pamoja, hatusahauliani, hatutupani

2. Natambuwa njia yangu, hata iwe na majani

Haijafa iko hai, taiandama andamo

Kwayo nirudi nyumbani

Yaumma nguvu ya umma, itaung`oa mfumo wa walaji wanyakuzi.

Nguvu itawasukuma, iwaponde humo humo, iwazibe na puumzi.Nguvu itawaandama, iwatie kwenye shimo

Citate By MKH

Share: