Habari

Breaking News- Polisi wenye silaha wavamia makao makuu ya CUF mtendeni

Makao Makuu ya CUF yaliyopo Mtendeni Zanzibar yamevamiwa na Magari na Polisi wenye silaha  tokea saa kumi na mbili jioni eti wanadai wamepokea taarifa kuwa kuna watu wanataka kuvamia makao makuu hayo kwa hiyo wapo hapo kwa kuyalinda

Pia wanasema wamepata taarifa mitaani kwamba kuna silaha sasa wanataka kuhakikisha wenyewe kama kweli maneno ya mitaani ni ya kweli (Polisi wameanza kusikiliza maneno ya mitaani)

Habari zaidi anasimulia Julius S.Mtariro

MTENDENI.

Polisi wameshabomoa Ofisi za Makao Makuu ya CUF Mtendeni, wanadai wanapekua ili kutafuta SILAHA zilizofichwa.

Hivi kweli CUF inaweza kuwa chama kinachotumia silaha? Yani wametupora ushindi 2015 chama kimetuliza wanachama wake, leo hii chama kinapekuliwa eti kina silaha??

Na ni chama gani hicho duniani kitakuwa na silaha halafu kizitunze ofisini? Naona enzi za kina MAHITA zimerejea, wakati ule siku moja kabla ya uchaguzi IGP Mahita akaibuka na visu akidai ni majambia yaliyoingizwa na CUF kuchinja wananchi.

Kama jeshi la polisi la leo linaendelea kujaribu kutumia propaganda za miaka hiyo ili kuumiza vyama vyetu na watu wake, tutapinga hujuma hizo kwa njia zote.

Vyombo vya dola vya nchi visijaribu kuwa chanzo cha kuleta vurugu na machafuko. Kuendelea kuvihujumu vyama vya upinzani ni jambo hatari sana, vyama vya upinzani vitakapokosa fursa ya kufanya kazi zake halali, nchi itaingia matatizoni.

Endeleeni kutupeleka ukutani

Share: