HabariZenjiLikiz

Breaking News! Taarifa nilizozipata hivi sasa kutoka visiwani Zanzibar

Malisa Godlisten

Taarifa nilizozipata hivi sasa kutoka visiwani Zanzibar ni kuwa Hoteli ya kitalii ya nyota 5, Konokono Beach Resort imeungua moto.

Mmoja wa wamiliki wa Hoteli hiyo ni Bi.Fatma Karume, Mwanasheria mashuhuri na mtoto wa Rais Amani Karume. Bado haijajulikana chanzo cha moto huo, lakini kuna kila dalili ni hujuma za kisiasa kutokana na misimamo ya Fatma kuhusiana na hali ya kisiasa visiwani humo. Ikimbukwe jana TLS walifanya kongamano kupinga Shein kuendelea kubaki madarakani na Fatma aliwasilisha mada.

Hali ya Zbar imekua tete na ya kusikitisha. Ni siasa za hovyo na za kijinga kuharibu mali kwa sababu mwenzio amekupinga kisiasa. Unachoma moto hoteli kubwa kama hii bila kujali watu wangapi watakosa ajira, serikali itapoteza mapato kiasi gani? Watalii waliokuwepo hotelini watasemaje huko kwao? Je hii haiwezi kuathiri sekta ya utalii nchini? Nalaani vikali wote waliohusika na tukio hili..

Share: