Habari

CCM ilegeze msimamo wake, isimamie sulhu

Hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Dr Abddallah Juma Mabodi akisema “hakuna mazungumzo tena kwa sasa, tukutane 2020 katika uchaguzi, washaona mambo yanakwenda vizuri wanaleta vidudu mtu… Tuliwaita mpaka wazee wetu wakatuzungusha sasa hivi wanataka nini hatuna muda tena…” Dr Abdalla ameeleza maoni yake pamoja na maoni ya Chama chake. Hapana shaka kwa chama tawala kama CCM kusmamia kauli zake kama hizi.

Unapomtazama Dr Abdalla Mabodi macho na sura yake havionyeshi kuwa ni mtu anayefaidika pale jamii ya Kizanzibar ikisuguana kwa mtazamo wa kisiasa. Anaonekana ni mtu ambaye yaliyowakuta mababu zetu yalikuwa yao wao kulingana na mazingira na time waliyokuwa nayo wao. IKiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu, hapa Dr Abdalla Mabodi kasoma. maendeleo ya technology, sasa hiv Dr Mabodi yuko na zama mpya, mjumuiko na muingiliano wa jamii wa rangi, tabaka, na jinsia tofauti. Pia Dr Mabodi yupo karne mpya ya 21, wakati mababu zetu walimalizia karne ya 20.

Yote haya yananifanya niamni na nimuone Dr Mabodi kuwa ni mtu mwenye mtazamo mwengine wala kwake hakuwezi kuwa na manufaa pindi jamii ya Wazanzibar ikiendelea kusononeka kwa msuguano wa kisiasa . Hivyo atasimama hima kuutafutia ufumbuzi na sulhu ipatikane.

Suala la sulhu siku zote linaanza na nia safi. Rais wa Afrika ya Kusini, Frederik Willem de Klerk (1989-1994), alinuwia kufanya mabadiliko makubwa yaliyopelekea jamii ya wa Afrika Kusini kuishi maisha haya wanayoishi leo. Aliondoa sheria za ubaguzi wa rangi, aliruhusu maandamano, aliviruhusu vyama vya kisiasa vilivyopigwa marufuku, aliwaachia huru wafungwa wa kisiasa akiwemo Nelson Mandela, nakadhalika. Yote haya ni kutaka kuijenga upya Afrika Kusini, yenye mchanganyiko wa rangi kuwa mng’aro mmoja, yenye makabila kuwa na utaifa mmoja.

CCM ipo kuwatumikia wananchi wake. Wananchi nao pale wanaposema wamechoshwa na msuguano wanatamani sasa hivi kuangalia muskabali wa watoto wao kielimu, kiafya na ajira, haina budi kuwasikiliza. Dr Mabodi pia akubali kulegeza msimamo wake kwa maslahi ya Wazanzibar, wamechoka.

Huwezi kuleta maendelea bila ya kuwashirikisha wananchi wenyewe. Laiti ingewezekana sio Zanzibar ingetoka kwenda Emirates kujifunza au kuomba msaada, wao wangejifunza kutoka kutoka kwetu. Kwani miaka 54 inatosha Zanzibar kuendelea na kutajika duniani kuwa ni miongoni mwa nchi zilizoendelea kama vile tunavyozitaja hizi zilizotualika. Lakini kikwazo kikubwa ni kuwa bado wananchi hawajatumika kikamilifu.

Sulhu inahitajika vyovyote vile iwavyo ili Zanzibar iweze kupiga hatua. Tusitosheke kwa kufaidi “vizuri”, bali tukimbilie kufaidi “vizuri zaidi”. Kama alivyofaidi De Clark, baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Arika Kusini aliendelea na nafasi ya Umako Urais huku jina lake likiingia kwenye kumbukumbu muhimu, pia akiiokoa nchi yake na janga la maafa ambalo lilikuwa linainyemelea.

Tukubali amani tunayojisifia ni kutokana na waZanzibar wenyewe, hivyo tusiwakatishe tamaa, wakateteresha amani yao. Tukae Wazanzibar kwa umoja wetu tujadili mambo yetu tukiwa wamoja.

Tagsslider
Share: