Habari

Chama cha Mapinduzi ccm kimemtaka makamo mwenyekiti ccm Z’bar Amani Karume Kurejesha Kadi na Wenzake

Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Vuai Ali Vuai.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemtaka makamo mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume na baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kurejesha kazi za chama hicho kutokana na kwenda kinyume na maadili ya chamana kutangaza sera zisizo za chama hicho.

cao jumbe Waziri Mansoor Yussuf Himid kurejesha kadi ya chama hicho kutokana na kukiuka maadili ya chama na kutangaza sera zisizo za chama chake.

Kauli hiyo imekuja kufuatia azimio la wajumbe wa chama hicho wa mkoa wa mjini magharibi waliokutana juzi mjini hapa na kuwashirikisha wanachama wapatao 400 ikiwemo wajumbe wa Halmadhauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Azimio hilo ambalo limesomwa mbele ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo limesema kwamba Mansoor akiwa na majukumu makubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na chama cha Mapinduzi CCM kama mjumbe wa NEC amekuwa akitamka kutaka Muungano wa mkataba hali ya kuwa akijua hiyo sio sera ya CCM.

Azimio hilo pia limesema kwamba Himid amekuwa akisema waziwazi kukataa muungano uliopo pamoja na kuwashawishi wananchi na wanachama wa CCM kuunga mkono suala hilo.

Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walifurahia baada ya kutolewa uamuzi huo kuonesha wanaunga mkono uamuzi huo wa kumtaka waziri Himid kurudisha kadi ya chama cha Mapinduzi.

“Tunaunga mkono maamuzi yalitolewa na viongozi wetu wa chama kwa sababu huyu muweka hazina wetu hivi sasa amebadilika sana” alisema mwanachama kiongozi mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini na kuongeza kwamba.

“Siku hizi wawakilishi wetu wamekuwa wakicharukwa sana kule barazani kwa hivyo azimio la leo litawafanya wengine warudi nyuma katika misimamo yao kwa sababu wote wanaokwenda kinyume na sera za chama tutawataka warejeshe kadi zetu” alisisitiza.
Katika vikao vya Baraza la Wawakilishi vinavyoendelea katika michango ya bajeti ya Wizara ya nchi ofisi ya rais Fedha mipango na Uchumi pamoja na wizara ya Katiba na Sheria, Himid alitamka bayana kuwepo kwa Muungano wa mkataba ambao utaiwezesha Zanzibar kuwa na dola kamili inayojitegemea na kuwa na kiti katika umoja wa mataifa.

Kikao hicho kilichowajumuisha mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Yussuf Mohammed na mwenyekiti wa wilaya Borafya Silima wakiwemo na wajumbe wengine wakiwemo wenye viti wajumbe wa halmashauri kuu aliwemo Waziri Machano Othman Said, Burhani Saadat na wengineo.

Himid alisema Zanzibar inahitaji kuwa na aina ya Muungano utakayoifanya kuwa dola kamili inayojitegemea,hatua ambayo itasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar.

Aidha kumekuwepo vipeperushi vinayoshabihishwa na CCM, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Mapinduzi Zanzibar Vuai Ali Vuai alisema kusema vipeperushi vinavyosambazwa katika kisiwa cha Unguja na Pemba havina uhusiano na chama cha Mapinduzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kuu Kisiwandui,Vuai alifafanua na kusema inasikitisha sana kwamba baadhi ya watu wasiojulikana wamechapisha vipeperushi mbali mbali ambavyo vinasambazwa katika mitaa mbali mbali vikiwa na sura ya chama cha Mapinduzi pamoja na kumuhusisha rais wa Zanzibar dk.Ali Mohd Sheni.

‘Napenda kuwajulisha wanachama na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi kwamba vipeperushi vinavyosambazwa mitaani havina uhusiano na chama cha Mapinduzi Zanzibar licha ya kuwahusisha viongozi wa ngazi za juu wa chama na Serikali’alisema Vuai.

Vuai alisikitishwa sana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukaa kimya huku jina la rais wa Zanzibar dk.Ali Mohd Sheni likitumiwa vibaya na kumuhusisha katika vipeperusdhi vinavyokwenda kinyume na sera ambayo yeye ndiyo iliyomuweka madarakani.

‘Nasikitishwa sana na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekaa kimya wakati jina na picha ya rais wa Zanzibar ikitumiwa vibaya katika vipeperushi vinavyomuhusisha muundo wa Serikali ya Muungano wa mkataba’alisema Vuai.

Watu wasiojulikana wamekuwa wakisambaza vipeperushi vya aina mbali mbali vikiwataka wananchi wa Zanzibar kuchaguwa muundo wa Serikali ya umoja wa kitaifa huku vipeperushi hivyo vikiwa na picha za viongozi wakuu wa Serikali akiwemo rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohd Sheni.

Baadhi ya vipeperushi hivyo vimewataka wananchi wa Zanzibar kuachiwa kupumuwa,vikimaanisha kuachiwa kuwa huru katika Muungano,huku vyengine vikiwashawishi wananchi wa Zanzibar kuchaguwa muundo wa Muungano wa mkataba ambao ndiyo utakaoleta maslahi ya wananchi wa Zanzibar.

Vipeperushi hivyo vimekuwa vikisambazwa katika maeneo yote ya Unguja na Pemba pamoja na vijijini huku vikiwa vimechapishwa kwa teknolojia ya rangi vikiwa na picha za viongozi wakuu wa serikali.

Vuai alisisitiza na kusema chama cha mapinduzi sera yake ni muungano wa serikali mbili ambao unakidhi mahitaji isipokuwa unakubaliana na kuwepo kwa marekebisho ikiwemo Zanzibar kupata fursa zaidi za kiuchumi zitakazoleta tija na maendeleo kwa wananchi wake.

Share: