Habari

CHOZI LISILOFUTIKA-

Na Ally Hilal

Damu yao
Machozi yao
Maumivu yao
Ni laana angamivu, kwa uliyowatendea

Aliyefanya
Aliyefurahi
Aliyeunga mkono
Naye hasalimiki, umati u nyuma yake

Cheka
Tembea
Furahi
Mzigo u juu yako, tena misumari moto

Ulisababisha;
Vizuka
Mayatima
Walemavu
Wakimbizi
Wote hawa unao, chini ya mkunazi

ALLY HILAL
P.O BOX 247
WETE-PEMBA
ZANZIBAR
26/1/2017
ahbenylal7@gmail.com

Share: