Habari

Chuo cha Fedha Z’bar kugeuzwa Chuo Kikuu

Khatib Suleiman, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kukifanya Chuo cha Usimamizi wa Fedha na Utawala kilichopo Chwaka wilaya ya kati Unguja kuwa Chuo Kikuu kwa lengo la kupanua taaluma ya mambo ya fedha.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango), Omar Yussuf Mzee aliyasema hayo
wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu mikakati ya SMZ kuongeza wataalamu wa mambo ya fedha na utawala.

Alisema chuo cha usimamizi wa fedha kimepata mafanikio makubwa katika kutoa elimu inayohusiana na mambo ya fedha na utawala na hivyo kuisaidia Serikali kupata wataalamu.

“Mipango yetu ya baadaye ni kukifanya chuo hiki kilichopo Chwaka kuwa sehemu ya Chuo
kikuu kamili…tunataka kuongeza wataalamu wa mambo ya fedha na utawala Serikalini,” alisema.

Alisema mipango hiyo ikifanikiwa Zanzibar itakuwa na wataalamu wa kutosha ambao
watafanya kazi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wengine kuingia katika sekta binafsi
ambayo ushindani katika mambo ya fedha ni mkubwa.

Mzee alisema tangu chuo hicho kilipoanza kutoa elimu ya mambo ya fedha katika ngazi ya
cheti na sasa stashahada, jumla ya wanafunzi 280 wamehitimu

HABARI LEO

Share: