HabariMakala/TahaririMaoni

CUF BARA YANGARA -MTATIRO

Hii makala imeandikwa na Mtatiro.
napenda kuwakumbusha viongozi wa CUF ambao sasa wengi wapo Zanzibar baada ya Lipumba kujiuzulu , pia juu ya kusubiri matokeo ya ya Zanziabr, na Hasa Maalim Seif atoe neno kuhusu CUF Bara ambapo ukawa umekipaisha na kukipatia wabunge na uwezo wa kuongoza halmashauri ikiwamo ya Tanga. Maalim atoe neno juu ya mafanikio haya makubwa ya chama ,

Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF
UKAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA SANA YA SIASA HAPA TANZANIA.

Hongereni sana Ubungo. Mimi sitakwenda Bungeni lakini mtu kama Kubenea anakwenda. Ni jambo kuu sana kwangu.

Kule Kinondoni CUF tuna kijana wetu mzuri anaitwa Mtulia Maulid, nikitoka ngome nakwenda kumuunga mkono kwenye majumuisho. CUF inaleta kijana machachari sana kutoka hapa Kinondoni.

Pale Temeke yupo Mtolea wa CUF huyu naye hadi sasa anaongoza. Kule Mbagala yupo Kondo Bungo wa CUF naye anaongoza. Ni faraja kubwa sana kwangu, vijana hawa wote wakawashe moto bungeni. Sisi tutawasaidia sana tukiwa nje ya bunge na huwenda ufanisi wao bungeni ukatokana na ushauri wetu huku nje.

CUF pia imetuletea SAKAYA, huyu ni samaki na huwezi kumfundisha kuogelea, kule kusini tayari tuna Kuchauka wa Newala, tuna Katani wa Tandahimba, tuna Bobali wa Mchinga, tuna —– Bungala wa Kilwa kusini, tuna Musa wa Tanga Mjini n.k.

Bado vijana kadhaa wa CUF pia wanaelekea kushinda kwenye majimbo mengine.

Siyo hivyo tu, CUF pia imepata na itaongoza halmashauri kadhaa ikiwemo Tanga Mjini, Newala, Tandahimba, Kilwa n.k. Haya ni maeneo ambayo tumepata madiwani wengi.

HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA CUF..

Tokea chama chetu kilianzishwa hakikuwahi kupata zaidi ya wabunge wawili Tanzani Bara na hakikuwahi kuwa na halmashauri hata moja.

Ndiyo maana mimi ni mtu nayeamini sana katika ushirikiano. Leo CUF inapata wabunge wengi bara, inaelekea kuongoza halmashauri kadhaa…Hii ndiyo faida ya kujitosa kwenye ushirikiano.

Tulipokuwa tunaanzisha UKAWA kuna watu walisema CUF itamezwa. Mimi nimeendelea kushikilia msimamo kuwa CUF haiwezi kumezwa kwani hivi sasa ina wabunge wengi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Chama chochote kinakuwa VIBRANT na kukua kinapopata wawakilishi wengi zaidi. Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CUF na UKAWA yenyewe.

UKAWA inapaswa kushughulikia changamoto zake zilizosababisha kukosa baadhi ya majimbo muhimu na kujiwekea utaratibu bora kwa uchaguzi ujao.

Mtatiro J,
Segerea.

Share: