Habari

CUF IMEDAI KUWA CCM IMEDHAMIRIA KUFANYA VURUGU KABLA YA KURA YA MAONI.

ZANZIBAR.

CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEDAI KUWA CCM IMEDHAMIRIA KUFANYA VURUGU KABLA YA UCHAGUZI WA KURA YA MAONI NA KWAMBA HAINA NIA YA DHATI YAKUPATIKANA KWA KATIBA MPYA.

TAARIFA ILIYOTOLEWA KWA VYOMBO VYA KHABARI NAKUSAINIWA NA MKURUGENZI WA HABARU ,UENEZI NA MAWASILIANO YA UMMA WA CUF NDUGU SALIM BIMANI IMEBAINISHA KUWA DALILI HIZO ZA VURUGU ZIMEANZA KUDHIHIRIKA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA VIONGOZI WAKE.

KATIKA TAARIFA HIYO CUF IMESEMA KUWA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI WAKUU WA MIKOA HAWAPASWI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZAKISIASA HIVYO VITENDO VYA VYA MKUU WA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA JUMA KASSIM TINDWA KUVAA MASHATI YA CCM KUTUMIA NAFASI YAKE KUTOA VITISHO KWA WANANCHI WENYE MSIMAMO TOFAUTI NA YEYE NA CHAMA CHAKE NI KINYUME NA UTARATIBU NA HAIKUBALIKI.

KUFUATIA KITENDO HICHO CHAMA CHA CHA WANANCHI CUF KIMEMTAKA RAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHD SHEIN KUMFUKUZA KAZI MARA MOJA KIONGOZI HUYO KUTOKANA NAKUKOSA SIFA NAKUPOTEZA HADHI YAKUWA KIONGOZI WA UMMA MWENYE ITIKADI TOFAUTI ZAKISIASA.

HATA HIVYO TAARIFA HIYO YA CUFIMEWATAKAWANANCHI KUTOKUBALI KUTISHWA NAKUREJESHWA NYUMA KATIKA MAPAMBANO YAKUIRESHA ZANZIBAR KATIKA MAMLAKA YAKE KAMILI KITAIFA NAKIMATAIFA.

CHAMA HICHO KIMEWATAKA WANANCHI BILA KUJALI ITIKADI ZAO ZAKISIASA KUIKATAA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NA WAFUASI WA CCM WAIPIGIE KURA YA HAPANA ILI KUYANUSURU,KUYALINDA NA KUYAENZI MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964.

Share: