Habari

Dk. Bashiru awasili Zanzibar kwa ziara ya kichama

August 17, 2018

NA IS-HAKA OMAR

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne visiwani humu kuanzia leo.

Dk. Bashiru anafanya ziara hiyo kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo Mei mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana kustaafu.

Akitoa taarifa ya ziara hiyo ya Katibu Mkuu huyo, Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu Taifa(NEC), Idara ya Itikadi na Uenezi CCM, Zanzibar Catherine Peter Nao, alisema CCM Zanzibar tayari kimekamilisha maandalizi yote ya mapokezi ya kiongozi huyo.

Catherine alisema katika ziara yake hiyo pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake na makundi ya kutoka taasisi za vijana visiwani humu.

Aliongeza kuwa ziara hiyo ya Dk. Bashiru itakuwa ni ya kikazi na kujitambulisha kwa wana-CCM ambapo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Katibu Mkuu huyo ambapo atazungumza na wanachama na wananchi kwa ujumla katika uwanja wa ofisi kuu Kisiwandui.

“Tunawaomba wanachama wote tujitokeze kwa wingi kushiriki mapokezi hayo ya kiongozi wetu mpendwa ambaye ni mara ya kwanza kuja tukitambulisha na kuzungumzia sera na masuala mbalimbali ya kuimarisha CCM na Jumuiya zake”, alisema Catherine.

Zanzibar leo

Share: