Habari

Dk. Shein atuma salama za pongezi Kuwait

February 25, 2018

NA RAJAB MKASABA, IKULU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi kiongozi wa taifa la Kuwait, Sheikh Sabah Ahmad Al-Sabah kwa kuadhimisha miaka 57 ya uhuru wa nchi hiyo.

Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaungana na ndugu zao wa Kuwait katika kusherehekea siku hiyo adhimu kwa taifa hilo.

Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimuhakikishia Sheikh Sabah Ahmad Al-Sabah kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Kuwait.

Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo na familia yake pamoja na wananchi wote wa Kuwait afya njema na sherehe njema katika kuadhimisha siku hiyo ya taifa.

Aidha alimtakia mafanikio zaidi katika kuendelea kuipatia maendeleo zaidi ya kiuchumi nchi hiyo kwa madhumuni ya kulinufaisha taifa hilo na wananchi wake.

Kuwait inaadhimisha uhuru wa taifa hilo kila ifikapo Februari 25 ya kila mwaka ambapo nchi hiyo ilipata uhuru huo kutoka kwa wakoloni wa Kiengereza mnamo mwaka 1961 chini ya jemedari wa taifa hilo marehemu Sheikh Abdallah Al-Salem Al-Sabah aliyefariki dunia mnamo mwaka 1965.

Zanzibarleo

Tagsslider
Share: