Habari

Dk. Sira: Wakandarasi tangulizeni uzalendo

September 16, 2018

NA ZUHURA MSABAH, PEMBA

WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, imewataka watendaji wa ujenzi wa barabara kuwa wazalendo na nchi yao kwa kutengeneza barabara zanye kiwango na zitakazoweza kudumu kwa muda mrefu.

Waziri wa wizara hiyo, Dk. Sira Ubwa Mamboya, alieleza hayo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea barabara ya njia kongwe Chake – Wete, ambayo ipo katika matayarisho ya kujengwa upya.

Alieleza ipo haja ya kuwatumia wakandarasi wa ndani baada ya kutegemea kutoka nje ya nchi, kwani kwa sasa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari imeamua kununua vifaa vya ujenzi ambavyo vitasaidia kujenga barabara.

Waziri huyo alisema, serikali imekuwa ikitumia pesa nyingi kwa wakandarasi kutoka nje ya nchi kwa kujenga barabara na hatimae wanapitisha muda wa makubaliano, huku barabara nyengine zikijengwa chini ya kiwango na kusababisha hasara.

“Katika ziara yangu ya kutembelea hii barabara kongwe, nimeona kuna vipande bado viko imara na vimejengwa toka mwaka 1989 havijaharibika na vilimejengwa na wakandarasi wetu wenyewe”, alisema Dk. Sira.

Zanzibarleo

Share: