Habari

Dr. Shein: Ada au Michango ya Elimu?

Kwanza Hongera Rais Shein na Wazanzibari woooote kw akuadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi.

Pili, nimesikiliza kwa makini sana hotuba yote (mara mbili au tatu) aliyoitoa Rais Shein katika kilele cha madhimisho ya sherehe za mapinduzi ya kutimiza miaka 51, pale Amaan stadium.

Kuna kitu sikukifahamu na nitamuomba Rais wetu anifafanulie – Je, elimu alikuwa inalipiwa hapa Zanzibar?
Kama ni hivyo, ni lini SMZ ilitangaza kuwa sasa elimu sio tena bure; au kw alugha nyengine ya mnasaba zaidi – Je, dhana ya elimu bure iliondoshwa (lini) na ilitangazwa wapi; alikuwepo nani? au BLM lilipitisha hilo? Je, wananchi tulijulishwa au…..?

Sasa kinachotolewa na wanafunzi ni kitu gani (ada au michango) iliyobuniwa na walimu wenyewe bila ya hata kupata ridhaa ya wazee au hata wizar inayohusika (yaani serikali)? Naomba ufafanuzi wenzangu.

Ninachikufahamu mimi ni kuwa walimu walianzisha hili (kuchangia) baada ya kushindwa hata kuwa na chaki za kuandikia maskulini, na pesa hawana, na wizara kushindwa kutimiza haya mahitaji muhimu kwao. Hapo ndipo ilipoanza hicho kitu kinachoitwa ‘michango’ au Dr.Shein anasema ‘ada’. Ilikuwa lazima mpaka leo wanafunzi wachangie hili, nafikiri kuanzia 3000 mpaka 5000 shs….skuli nyengine kwa mwaka mkapa elfu 12, na ushei. Almuradi michango au ada zitaendelea; na walimu sifikiri kama wataridhia kauli hii ya Dr.Shein.

Huko nyuma, Dr.Shein aliwahi kutoa amri kuwa ‘waja wazito wanaokwenda kujifungua hosp.pale mnazi mmoja – wasilipishwe’. Kauli hii pale pale ilipingw ana waziri wake mdogo wa afya, bi.sira ubwa mwamboya. Mpaka leo waja wazito wa waja wepesi tunalipa kuanzia huduma ya kunua daftari (cheti) mpaka X-ray au utra sound, na hata kuingia pale hosp unalipia, imekuwa kama vile kuigia disco tech/ukumbi wa muzik — pale hapana bure tena.

Ninavyoona ni kuwa hii ni siasa ya Dr.Shein kuelekea 2015, ili tumchague tena na tena. Hilo si tatizo, wewe utapata tu, ukishinda au usishinde — maana tumeshaaambiwa na akina Salmin Awadh Salmin kuwa ‘hata kama tutapiga kura mpaka vidole vikatike basi Zanzibar haitoki mikononi mwa CCM’. na lugha kama hizo……..na mengine mengi waliyosema akina Shaka, Haji Omar Kheri, Balozi Iddi n.k.

Hbeu tuangalie – hali halisi ya maskuli yetu…..idadi ya wanafuzni ni kuanzia ni kuanzia 60 na ushei, pale mwanakwerekwe, mabanda ya zamani ya maonyesho, sasa yamegeuzwa kuwa skuli — kuna mwanakwerekwe A, B, C,D….lakini kila darasa moja linasoma madarasa mawili (wanaolekea huku ni darasa la sita B, na kinyume chake wanasoma daasa la sita A — mfano). Deskmoja na watu wawili, wanakaa wanne mpaka watano…..na hali ndio kama hiyo jamani. Je, hii tutalittaua vipi?

Chengine ujenzi wa skuli — SMZ imeamua kujenga skuli kubwa hata kama hakuna wanafunzi wa kusoma, mfano — makunduchi, lakini wilaya ya magharibi pekee inahitaji skuli kama 15, ni wilaya yenye wakaazi wengi wengi kuliko zote Zanzibar kwa mujibu wa sensa ya watu 2012.Nimetaja Makunduchi kwa sababu wakakti wa Maalim Haruna, kama waziri wa elimu, alilazimisha ujenzi wa skuli huko just kuvutia ‘maendeleo’ katika jimbo lake ilhali hakuhitajiki skuli. na kuzipiga panga pesa ambazo zilihitajika kwa wahitaji wa skuli, kwa mfano, wilaya ya magahrib. SMZ ilimuachia kukamilisha interests zake wakati nchi inaumia.

Hii ndi hali halisi ya hapa Zanzibar, ubinafsi, kuvirigiza maneno (ada au michango) ya kuwazuga zuga wananchi kwa kuambiw akuwa ‘serikali inawaonea huruma ilhali inazidi kuwaumiza.

Kwa fikra zangu mimi, kauli hii ya Dr.Shein kuhusu kulipia mitihani, na kufuta ‘ada/michango’ ni ya kisiasa zaidi ni turufu ya kutaka kuchaguliwa 2015, kulainisha mitambo, kuwalainisha wananchi ili wamuone ‘hodari na mwema’ baada ya mtafaruk wa maisha.

Ukisikiliza ile hotuba yake, utapata picha kuwa Zanzibar ni nchi tajiri sana, na hakuna umasikin.

Ashak Kiongozi, mengine nimeyawacha kiporo, na hasa sijajua kama ada hii ni ya ‘umma au …..’kama vile Escrow tu.

Share: