Habari

Dr Shein ateuwa watendaji wa Mawizara

Kufuatia mabadiliko ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika hivi karibuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilsha wadhifa baadhi ya watendaji wakuu katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:

1. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
Bwana Shaaban Seif Mohamed ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

2. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
Dkt. Idrissa Muslim Hija ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

3. WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE

i. Bibi Khadija Bakari Juma ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

ii. Dkt. Saleh Yussuf Mnemo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayeshughulikia masuala ya habari.

iii. Dkt. Amina Ameir Issa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anaeshughulikia masuala ya Utalii na Mambo ya Kale.

4. WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

i. Bwana Omar Hassan Omar ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

ii. Bwana Amour Hamil Bakari ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo

5. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

i. Bibi Maryam Juma Abdalla Saadalla ameteuliwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi

ii. Bwana Ahmad Kassim Haji ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi anaeshughulikia masuala ya Kilimo na Maliasili

6. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

i. Bwana Juma Ali Juma ameteuliwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara na Viwanda

ii. Bwana Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

7. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO

i. Bibi Fatma Gharib Bilal ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto

ii. Bibi Maua Makame Rajab ameteuliwa kuwa Naibu katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Kazi na Uwezeshaji.

iii. Bibi Mwanajuma Majid Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Wazee, Wanawake na Watoto.

8. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

i. Bwana Ali Khalil Mirza ameteuliwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati.

ii. Bwana Tahir M. K. Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati

9. BODI YA MAPATO YA ZANZIBAR

Bwana Joseph Abdalla Meza ameteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).

10. BENKI YA WATU WA ZANZIBAR

Bibi Khadija Shamte Mzee ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendajii wa Benki ya Watu wa Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza tarehe 12 Machi 2018.
Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu waliotajwa pamoja na Kamishna wa Bodi ya Mapato wanatakiwa waripoti Ikulu siku ya Jumanne tarehe 13 Machi 2018, saa 2:30 asubuhi tayari kwa kuapishwa.

(Dkt. Abdulhamid Y. Mzee)
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi
Zanzibar.
TAREHE 10 MACHI, 2018

Zanzinews

Share:

8 comments

 1. Ashakh (Kiongozi) 12 Machi, 2018 at 11:36 Jibu

  Nimependa kitu kimoja tu; hii kuita Bibi na Bwana kuwa ndio title zao.
  Ilikuwa huu utamadumini umanza kupotea , tunaitana title za kuiga. Kukulia kwangu nasikia Bwana Fulani na Bibi Fulani, lakini kama kawaida yetu ilianza kusikika tofauti. Vyema kuurudisha utamaduni huu.

  Tumeanza watunzi wetu wengi sasa hivi wanatunga kwa lahaja ya Kipemba, inapendeza. Wako wanapenda kuiga lahaja nyengine kama vile “ongea” “hela” wakati sio lugha sanifu.

  • Ashakh (Kiongozi) 12 Machi, 2018 at 15:29 Jibu

   Nafikiri itakuwa kwenye Wizara ya Habari, Utalii, na Mambo ya Kale.

   Wakati ilipaswa iwe kwenye wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

   Kwa muona wangu nikapanga hivi;
   1) Wizara ya Michezo, Utamaduni, Sanaa na Mambo ya Kale
   2) Wizara ya Biashara, Viwanda na Utalii
   3) Wizara ya Kazi na Jinsia (wanawake, wanaume, wazee, watu wazima, vijana, watoto, walemavu (vipofu, viwete, viziwi) )
   4) Wizara ya Elimu na Mafunzi ya amali
   5) Wizara ya Habari na Mawasiliano
   6) Wizara ya Ujenzi , nyumba , na usafirishaji
   7) Wizara ya Ardhi, Maji na Nishati
   8) Wizara ya Fedha na Mipango
   9) Wizara ya Kilimo, Maliasili, mifugo na uvuvi
   10) Wizara ya Afya
   11) Wizara ya Ofisi ya Makamo wa Pili
   12) Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi na Vokosi
   13) Wizara ya Ofisi ya Rais Katiba
   14) Wizara ya Ofisi ya Rais , BLM

 2. Piga nikupige 12 Machi, 2018 at 21:46 Jibu

  Dkt Shein unamuogopa Dkt. Abdulhamid Y. Mzee, Kma kuna kiongozi asiye kuheshimu huyu ndiye nambari moja na wewe mwenyewe unalijuwa hilo kwanini unashindwa kumuondoa?

  Bwana huyu popote utakapo muulizia utaambiwa huyu kiumbe ni mkorofi anzia kwa Wawakilishi,Mawaziri, Viongozi mbali mbali wa Taasisi za Serikali pamoja na Wananchi wa kawaida wengi wao wanalalamika kutokana na ukorofi wa bwana huyu. Kama huamini unda tume huru ichukuwe maone ya wananchi kuhusu tabia za kimbe huyu, nadhani majibu yake utayapata.

  Kiumbe huyu hata ukampelekea barua anajifanya kama haioni, hata mwonekano wake kwenye watu unamouna kwamba yuko tofauti na wenzake ,hacheki hasa kwenye kioo cha TV ndio usiseme unamfaidi yaani ukorofi wake umeibadilisha mpaka sura yake.

  Kigezo cha mtu mwema kwenye dini ya kiisilamu ni kutajwa kwa wema mtu huyo,, na endapo utaikuta jamii kubwa inamtaja mtu kwa ubaya basi mtu huyo ubaya basi bila shaka mtu huyo atakuwa ni mbaya kweli.

  Dkt. Abdulhamid Y. Mzee “Tunakuusia mche Mungu kama tunavyo ziusia nafsi zetu, Dunia ni mapito wacha ubaya wa nafsi, hautokupeleka popote isipokuwa kwenye maangamizo.
  Mzee umezidi kila mtu anakuchukia kiumbe wewe, Jitafakari badilika kumbuka kuna na Akhera.

 3. Ashakh (Kiongozi) 13 Machi, 2018 at 06:43 Jibu

  Piga nikupige

  Hayo yote ulieleza mie kwangu ni madogo.

  Kubwa ni kwenye majukumu yake. Yeye ni Katibu wa makatibu, msimamizi mkuu wa watendaji. Msimamizi mkuu wa public services.

  Hivi inakuwaje kila mkutano , alipo Dr Shein naye yupo. Akiweka mguu Dr Shein naye achupisha wake. Kwenye kampeni yupo. Au ndio public service majukumu yake?

  Anachotakiwa ni kuisimamia public service sio kumfuata Rais anapokwenda

 4. zamko 14 Machi, 2018 at 16:17 Jibu

  He is the same as Sefu Ali Iddi. These two People they are the one put zanzibar into an economoc crisis.

  Prices of basic goods and services its sky rocking

Leave a reply