Habari

Dr Shein kwa hili nakuunga sikio, Ela…..

Dr Ali Mohamed Shein , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesikika akikemea vikali tabia ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano kwa kile alichokiita kuchanganya mambo ya muungano na yasiyokuwa ya muungano, na kuyafanya kuwa ya muungano. Sinabudi kwa msimamo wa Rais juu ya kadhia hii KUMUUNGA SIKIO (sio mkoo kama tulivyozewea). ELA kwa hili Dr Shein ni kusudi yako.

Nitatowa ufafanuzi baadae kidogo wa KUKUUNGA SIKIO na KUSUDI YAKO, kwanza tuangalie kile Dr Shein ulichosema kama hivi:

“Nataka niwakumbushe wenzangu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mawaziri , Manaibu Mawaziri na Watendaji wote wa pande mbili. Kwamba mambo yanayohusu mambo ya muungano yasifanywe na upande mmoja. Mambo ya muungano yafanywe na pande zote mbili. Mmoja akivuta kwa upande wake, mwengine akilegeza au hashirikishwi inaondosha uwezo na nguvu ya nchi yetu kwamba tuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili ni muhimu sana. Tusifanye hata siku moja, upande mmoja ukifanya kidogo mwengine akafanya sana.

Madhali ni Jamuhuri ya Muunngano wa Tanzania letu sote. Nataka hili nilisema waziwazi ili tutanabahi kwamba mambo ya muungano yabakie kuwa ya muungano yasiwe ya upande mmoja, yawe ya pande zote. Na wanaoyasimamia haya wasimamie vizuri. Nayasema kwasababu nayajuwa vizuri, nimeyafanyia kazi mambo ya muungano miaka tisa na nusu, nayajuwa.”

Dr Shein, Rais wa Zanzibar, hayo ndio maneno yako.

Nimepekenyua kutaka kujuwa ni kipi kilichokusuma hata leo hii kutoa kauli kama hii. Wakati miaka tisa na nusu unayajuwa vizuri mambo ya muungano, wakati kwa muda wa miaka saba baadae ulikuwa ukisema tayari kero zote zishatatuliwa, mambo ya muungao sasa yako safi. Kipi kilichokusibu Rais wetu.

Nimepata sababu zifuatazo kwamba zimekuudhi, inaweza kuwa zote au baadhi yake, ingawa hukuzisema ila ndani ya nafsi yako nambie kuwa ni sababu kadhaa na kadhaa, nyoyo zetu Dr Shein zasemezana. Mambo yenyewe nitayaweka kwa orodha kama ifuatavyo;

i) kuangushwa front line au front bench yako yote kwenye uchaguzi mkuu wa CCM uliofanyika December 19, kisha ukaletewa wengine hata sio Wazanzibar kuwa ndio viongozi wa CCM Zanzibar, hili lilikukirihi ndani ya nafsi yako.
ii) Mgao wa Bank Kuu ya Tanzania, hadi hivi sasa hujaambulia hata shilingi wachilia mbali 4.5% ya faida iliyopatikana. Ingawa haki yetu hasa ni 11%. Pia kuna fununu kuwa ile faida iliyotangazwa ilikuwa kimakosa, badala yake, na kiukweli nikuwa BOT imepata hasara. Huu ndio ujanja wa nyani kula hadi majani.
iii) Kwamba umechukizwa na kitendo cha Amiri Jeshi Mkuu kushindwa kuwaaga (wananchi na majeshi yako 9) waliouwawa vitani. Kuwa hawakuthaminiwa wengi wa Zanzibar wamethamini wale wachache wa Tanganyika.
iv) Hii tabia ya hivi karibuni kwa Mawaziri wa Tanganyika, Khamis Kigwangwala na Willium Lukuvi, kufanya mambo siyo ya muungano ya kujichukulia maamuzi ya kimuungano.
v) Zanzibar kuvuliwa uanachama wa Chama cha Mpira cha Afrika (CAF)
vi) Chaguo lako la mgombea Urais kukurithi mwaka 2020 ukiondoka, linaelekea kukataliwa na baba mwenye nyumba
vii) Pressure ya kurudisha haki ya watu, inayodaiwa kuporwa kwenye uchaguzi mkuu October 2015

Dr Shein, zote hizi au baadhi ya sababu nilizotaja hapo juu inasadikiwa ndio iliyokupa ujasiri wa kuyatamka maneno haya.

Nimesema NAKUUNGA SIKIO kwa vile ni maneno mujarabu umeyatowa bila kutafuta maneno wala kufanya utata wa mdomo. Maneno ambayo kila Mzanzibar anaona ufakhari kwa kiongozi wao kuyasema kupinga dhulma zinazofanywa waziwazi kupitia jini huyu Muungano. Imani ya Wazanzibar wote, mimi wa kwanza, pindi ukiyasema haya na kuyafanyia kazi yatanyanyua hadhi yako. Nimekuunga sikio kubakia kuyasikiliza tu, yapitie sikio moja yatokee sikio jengine. Utakapoyatekeleza nakuahidi hapo NITAKUUNGA MKONO.

ELA YOTE HAYA, Dr Shein kunataka mwenyewe. Miaka 9.5 upo kwenye mambo ya muungano, jumlisha miaka 7 upo ubavuni wa mambo ya muungano, jumla ni miaka 16.5 hivi hadi leo hii tusikie kuna kero za muungano. Aidha hukuwa ukishughulika nayo au hukutaka kuyafanyia kazi. Au ulikuwa uko weak mbele yao.

ELA ukiziangalia hizo sababu zote hapo juu, yote uliyataka weye. DR Shein mwaka 2010 umeingia madarakati ukiwa Rais wa Zanzibar ulikuwa ukiwaongoza Wazanzibar 98%. Mwaka 2015 unaendelea na urais wako unawaongoza Wazanzibar 46%, jee huku si umeyataka mwenye. Iko wapi 52%?

Mwaka 2010 ulipokuwa Rais uliunda serikali yenye talent staff, ELA mwaka 2015 umewatupilia mbali wale talent staff. Yupo wapi Asaa Ahmad Rashid, ambaye alikuwa Katibu Bunge la Katiba. Wapo wapi Othman Masoud (Ex Mwanasheria), Yahsa Khamis Hamad (Ex Katibu BLW), Dr Omar Dadi Shajak (Ex Katibu MKR), Juma Amour (GMD PBZ), Rashid Ali Salim (Naibu Katibu BVM), waswaghiruhu wakabiruhu. Badala yake unaendelea kukumbatia watu corrupt wala hawakusaidii kwenda mbele isipokuwa kutengeneza ring la kuwa na mgombea wao 2020.

Dr Shein umemchagua Julian Rafael kuwa Naibu Governer kwa misingi na matumaini gani. Hivi hakuna watu waliokuwa experienced and competent in banking hata umpeleke huyu Julian. Huoni kuwa uwezo wake mdogo, uzowefu hana na mwisho anatetea maslahi mapana ya mother land yake. Hiyo ndio sababu ya kuukosa 4.5% mgao wa BOT.

ELA wakumbuka ulipomtuma Sh Saleh Alkabhi, Kadhi mkuu, aende akazungumze na masheikh wengine. Jee yale aliyokuletea vipi uliyafanyia kazi? Unapowashirikisha watu kama hawa ujuwe wako karibu na malaika, na M/Mungu anawasikiliza. Umempuuza.

Tokea 2010 bado imani yangu ipo kwako Dr Shein kwamba unaweza (ukitaka) kuyakabili matatizo yote ya muungano na kuyapatia ufumbuzi, ELA lazima usafi nia yako, kisha urudi ufanye kazi na Wazanzibar wenzako. Kujikalia na kusema maneno kama haya tu hakusaidii lolote, kwani hao unaowambia watakuwa kama mimi, yaingie sikio moja yatokee sikio jengine. Rudi kwa Wazanzibar ufanye nao sulhu, ukubali yaishe kisha tusonge mbele.

ELA ni kawaida ya viongozi wetu wote inapofikia term yao ya mwisho ya uongozi husema na wengine kufanya hasaa kama hivi. Tukianzia Sh Aboud Jumbe, Dr Salmin Amour, Aman Abeid, na leo Dr Shein. Wote walikuwa mashujaa kuukosoa muungano wakiwa wamebakia miaka michache kufikia mwisho wa uongozi wao.

Tagsslider
Share:

5 comments

 1. Piga nikupige 5 Januari, 2018 at 17:58

  Kwa kauli uliyo itoa Dr. Shein unapaswa uwe na hadhari kubwa kuhusu usalama wako, hjasa masuala ya chakula na maji,na mambo ya ki kolimba kolimba. Kazi kwako.

  Usimuamini tena mtu yeyote kwa jambo lolote. Kwa sababu jamaa zetu ukitaka wakuchukie sema ukweli (itetee Zanzibar) hapo watakuona adui wao mkubwa hata kama uliishi nao kwa mashirikiano ya kila wanalo litaka.

  Lakini mbona Dr. Shein Umekwenda mbali wakati hata Mawaziri wako ulio wateuwa wewe mwenyewe hawakuheshimu? Mbona umeshindwa kuwachukulia hatua? Waziri wako Salama Aboud amekuwa mwiba kwa wananchi ni msanii kupita kiasi amegeuka kuwa kikwazo cha kuzuwia haki za watu zilizo wazi. Au wewe ndio unamtuma afanye hivyo?

  Tunakuomba nenda wizarani kwake kakaguwe utakuta mafaili kibao ya maombi ya watu kupatiwa haki zao, huu ni mwaka au zaidi hajasaini chochote, wafanyakazi wa Wizara wanalalamika. Au na hili hulioni? Basi unashindwa hata kulifatilia hili wizarani kwake? Ndio maana ikawa hakuheshimu, hafati maagizo yako wala hakujali.

  Ukitaka kujua zaidi kuhusu Salama Abuod email yangu ni silimajuma@outlook.com

  Kwa vile nasema ukweli nimejitolea sadaka. Tunakuomba uanze na salama Aboud asikudanganye hana anacho kifanya zaidi ya ukorofi na uongo, anahangaisha watu kwa nini.

 2. rasmi 5 Januari, 2018 at 18:24

  Dr Shein na wenzake tunachokitaka ni Zanzibar yetu tu, munakataliwa kwa kauli na vitendo na hao ‘wenzetu’ hamusikii?
  Usitishie nyau tu kama ‘wakiukata tutawasha vibatari.’ Fanyeni kweli muone kama Wazanzibari hawatokua pamoja nanyi.
  Dharau zao mpaka lini kwa wala urojo…!?

 3. Tengoni 6 Januari, 2018 at 04:39

  Kauli za kawaida, za kuaga kwa marais wa Zanzibar, wanapoingia huwa wakali juu ya wausemao muungano , lakini wanapoona jua limewatulia na wataishia kutupwa kama condoms, ndio huanza kutowa kauli zinazopendwa na wazanzibari walio wengi, ili kujisogeza kwao baada ya kustaafu. Sheni anajuwa uzuri alipo commando salmini, mpweke hapitiwi na marafiki, wala wapambe na huko Dodoma wala hatajwi tena, yuko wapi karume, anaonekana kinyago na ccm, kwa palipo baki Sheni utaishia huko huko walikoishia kina commando.

 4. abuu7 6 Januari, 2018 at 11:09

  Zanzibar’s haina haja ya vyama …zanzibar ina haja ya mamlaka kamill
  Hili dola kubwa kwa bara la afrika. Lakini tumefunikwa kwa kila kitu.tulikuwa tuna silaha ya mashekh wako wapi sasa. Tilikuwa tuna silaha za biashara ziko wapi sasa.
  Hayo maendeleo mnayoyaona ni danganya toto.
  Nimeona kwenye news inasema wale majeshi wa tanganyika na wa dolat zinjibar eti terorist kutoka uganda ndio walio vamiya. 🤗🤗
  Dr shen . Panga siku kutana na maalim . Na uhakika mnawajuwa viongozi wote nuksi kutoka CUF na CCM…wazibitini tangazeni sasa zanzibar ina mamlaka kamili na hakuna mungano kwa sasa .
  Tanganza duniya new kiti UN.mwisho ndio tutakuja kwenye mungano tena wa piriod

 5. Papax 6 Januari, 2018 at 13:08

  Dk,shen, kajamba kwenye maji ushuzi kauskia mwenyewe, anataka haki ipi apewe na jamuhuru , je hasaminihuu uluwa mliopewa wz znz, ya kuwa na serekali ya kiuongo, uwongo uongo, jamuhuri ya tz, ni moja na znz, ni moja ya mikoa ya tz, mumepewa mamlaka mujiendeshe , hamuwezi bkujiendesha kaziyenu kulalamika tu, waznz, sio sifa yenu uongozi nyie ni wakuongozwa tu , mungua aubariki mungano na serekali moja mungu atuletee , tukukateni kidomodomo

Leave a reply