Habari

Dr Shein, usajili wa meli unafanyika kisheria

Leo Rais wa Zanzibar Dr. Shein, alipoulizwa kuhusu kusitishwa na kuzuiliwa kusajili Meli hilo swala analizungumziaje? Amesema Usajili wa Meli unaiingizia Zanzibar Kipato. Na ni swala ambalo linafanyika Kisheria.

Amesema kama wanaona Sheria hazifai wazifute au wazirekebishe ila hadhani kama kuna mtu anaweza kuwazuia kuhusu usajili kwani ni swala wamelifanya miaka mingi tangu enzi za Karume.

“Sisi tulianzisha wenyewe Kampuni yetu ya Usajili wa Meli, Hili la kusajili Meli si jambo jipya, na nchi Duniani haya yanafanyika, Na mimi sidhani kama Zanzibar itazuiliwa kuregister, sidhani kama lipo hivyo, Mimi sijasikia hivyo, Mimi ninachojua kuna timu za Wizara za Serikali mbili zinazungumza na mazungumzo yatakavyo kwenda mimi nitayajua. Sidhani kama Zanzibar itaambiwa Isisajili. Kinachofanyika sasa hivi, labda kwa muda Kusimamisha kwanza ili kufanya survey Vizuri.

Sisi Zanzibar bado tunaregister, NI jambo la kisheria la Zanzibar na hili jambo halipo katika mambo ya Muungano, si swala la Muungano, kwahiyo kwanini Zanzibar inyimwe nafasi hiyo?

Makosa kama yamefanyika hatukufanya sisi, hao wenye Meli ndio wamefanya Makosa, Hao Vijana wanaosajili hawajui. Kama sheria zetu hazina nguvu basi tutazipa nguvu sheria zetu ili wasituchezee kwa mara nyingine. Na hilo linaweza likafanyika”. Amesema Dr. Shein.

Kauli hii imekuja siku chache baada ya rais wa Jamhuri ya Muungano John Magufuli kupiga kusitisha Usajili wa meli kutoka nje.

Share: