Habari

EPISODE zisitutowe kwenye mada, Hoja ya Zanzibar na mamlaka yake ipo mezani

Kuna mdudu aitwa kupe. Mdudu huyu hukaa kwenye wanyama ikiwa ndio machumo na muendelezo wa mfumo wa maisha yake. Tofauti na wadudu wengine ambao wanakuwa na eneo la kuishi na eneo jengine mbali la kutafuta kujio, kupe yeye ni hapohapo, nyumba, kijio, choni, nk.

Wazanzibar tushikilie na tuendelee kujadili hoja zetu tulizokuwa nazo kabla ya EPISODE ya jana iliyotokea hapo Mtendeni. Tufanye kama vile hatujuwi au hakujatokea kitu. Kuna mengi tulikuwa nayo kabla ya jana, kama lile la kuzuiliwa Zanzibar kufanya usajili wa meli za nje, wazo la Prof Kabudi kwamba Rais wa Muungano ana haki zote hata kuingilia mamlaka ya Zanzibar pamoja na kuwapa amri na maagizo mawaziri wa Zanzibar, Hoja ya Mwakilishi Nadir, Hoja ya passport, hoja ya kuziliwa makontena kuingia Zanzibar kutokea Mombasa, nakadhalika

Hizi siasa za kitoto (propaganda) zisizo mashiko imepitwa na kitoto. Watu wana SPIN DOCTORS pale wanapotaka kubadili muelekeo wa jamiii. Ukiachilia mbali wataalamu kama hao pia hutumia gharama kubwa ya fedha kutumiza azma yao. Sio kumnunua mtu kwa kil ya mchele, pea ya kanga, kitenga, fulana amma kofia.

Pia propaganda sio itumike kwa muda wa siku moja ndio imekwisha bali ni investment ya miaka kadhaa inayokuja. Wende wakajifunza propaganda ya Alqaida, nk. Sio unafanya upekezi dakika 10 umekwisha ukidhani hiyo ndio propaganda ya kuzima madai na hoja zetu.

Mkoloni anaamini haya yote yanayofanyika Zanzibar kuwa yanatokana na chama cha Wananchi CUF, kumbe ni tofauti. Binafsi sikubaliani na baadhi ya madai ya CUF au matendo yake. Hata mukifanya upekezi kwa Chama cha CUF badi Wazanzibar wapo na madai ya nchi yao, nalo ni moja tu UKOLONI UFIKE MWISHO WAKE. Tena basi hatuto toka kwenye line ya kujadili na kuukataa muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar.

Share: