Habari

Furaha za Kisonge sio muda Mrefu zitawatumbukia Nyongo CCM/SMZ.

Kwa Kiswahili ni thuluthi mbili…kwa kihesabu ni 2/3

Hakuna shaka kua katiba hii ikipita hakuna tena kwa Zanzibar walilobakishiwa Zanzibar kua hili si la Muungano na WTanganyika, Na kama lipo basi lisemeni ni lipi na lipi si la Muungano kama lipo? Wametengwa ccm/Smz na wakategeka sasa furaha zao kuona kua wanawakomoa Cuf na kuwa kejeli , mimi naona zaidi wanajikomoa wao.

Nenda deep katika vifungu vya katiba hii waitayo mpya utaona imeramba kila kitu kwa Zanzibar na kukingiza katika mambo ya Muungano, sasa lipi wekeni wazi na musehe hili tumeashiwa si lamungano? wamekula Bahari mpaka nchi kavu (ardhi) anga na Mawasiliano hayo yote ni eneo la jamuhuri ya Muungano, mambo ya nje na pesa za kigeni, leseni za viwanda vikubwa biashara na Bandari, Kodi za Mapato ,Elumu ya Juu etc.

Sasa lipi twambieni lisilo la Muungano? hapa wame pigwa changa la macho na hayo mafuta ikiwa ardhi na Bahari na eneo late la Zanzibar ni la Muungano hayo mafuta yatatoka kweli kwenye uzio huu walio zungumshiwa?

Kwa hio kama ccm/smz nikuwakomoa cuf Zanzibar(Wapinzani) basi zaidi wanajikomoa wao au ndio wameamua na litote ili tuwakomowe cuf tu basi hilo ni jambo jengine ,lakini kwa kusema kua Katiba hii Zanzibar emewabakishia kua hishi na hishi hakimo katika Muungano basi ccm/smz munajidanganya na kujifurahisha hakuna walicho bakisha Watanganyika kwa Zanzibar.

YAPITIENI VIZURI VIPENGELE ALIVYO VIKATAA MWANASHERIA WETU ,ZAMENI DEEP MUTAONA LOCK WALIZO ZITIA WTANGANYIKA HAWAKUASHA KITU.

Vifuatavyo chini ni vifungu ambavyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alisimama kuvikataa katika Bunge la Katiba kwa maslahi ya Zanzibar.
Pia alikataa Orodha ya Mambo ya Muungano.
Nimeona nichukue bidii ya kuviweka pamoja ili viwe wazi zaidi na isaidie usomaji mzuri na ulio rahisi kwa watu wengi.

Eneo la Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni:
(a) eneo lote la Tanzania Bara, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari
ambalo kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Tanganyika
pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka; na
(b) eneo lote la Zanzibar, ikiwa ni pamoja na eneo lake la bahari ambalo
kabla ya Muungano lilikuwa likiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
pamoja na maeneo mengine yatakayoongezeka.
(2) Rais wa Jamhuri ya Muungano atakuwa na mamlaka ya kuigawa
Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengine na kwa upande wa Zanzibar, Rais anaweza kukasimu mamlaka hayo kwa Rais wa Zanzibar.
(3) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), Bunge litatunga sheria
itakayoainisha na kufafanua mipaka ya eneo la Jamhuri ya Muungano.

——–

Ukuu na utii wa
Katiba

9.-(1) Katiba hii ni sheria kuu katika Jamhuri ya Muungano kwa mujibu
wa masharti yaliyowekwa na Katiba hii.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), endapo masharti ya sheria
yoyote itakayotungwa na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria
yatatofautiana na masharti ya Katiba hii, masharti ya sheria hiyo yatakuwa batili na yatatenguka kwa kiwango kile kinachotofautiana na masharti ya Katiba hii.
(3) Mtu yeyote, chombo au taasisi ya Serikali, jumuiya, wakala yeyote
na mamlaka binafsi zitakuwa na wajibu wa kuzingatia na kutii masharti ya
Katiba hii na sheria za nchi.
(4) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo cha dola
au ofisa wa Serikali ni sharti ufuate na kuzingatia masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba sheria, mila, desturi au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti ya Katiba hii utakuwa batili.
(5) Serikali itaweka utaratibu wa kuwawezesha wananchi kuifahamu,
kuilinda na kuitii Katiba hii.

——-

Muundo wa
Muungano

70. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa na muundo wa Serikali
mbili ambazo ni:
(a) Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na
(b) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

——–

Utekelezaji wa
shughuli za
Mamlaka ya Nchi

71.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano
zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,
vyombo viwili vyenye mamlaka ya utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye
mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; vyombo vyenye mamlaka ya utoaji haki vitakuwa ni Mahakama ya Jamhuri ya Muungano na Mahakama Kuu ya Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.
(3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma katika Jamhuri
ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa madaraka juu ya shughuli hizo
baina ya vyombo vilivyotajwa katika Ibara hii, kutakuwa na Mambo ya
Muungano kama yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba hii na pia kutakuwa na mambo yasiyo ya Muungano, ambayo ni mambo mengine yote yasiyo ya Muungano.
(4) Kila chombo kilichotajwa katika Ibara hii kitaundwa na kutekeleza
majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika Katiba hii.

——-

Mamlaka ya
Serikali ya Jamhuri
ya Muungano

72. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji
katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara.

——

Mamlaka ya
Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar kwa
mambo yasiyo ya
Muungano

73.-(1) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka na haki
juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.
(2) Bila kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, katika kutekeleza
mamlaka yake chini ya ibara ndogo ya (1), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa.
(3) Endapo, katika kutekeleza mamlaka na majukumu yake kwa mujibu
wa Ibara hii, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahitaji kupata ushirikiano
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi ya kikanda au kimataifa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza kufanikisha uhusiano au ushirikiano huo kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na sheria itakayotungwa na Bunge.
(4) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria itakayoainisha
na kufafanua:
(a) majukumu na mipaka ya utekelezaji wa mamlaka ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu
uhusiano au ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(b) utaratibu wa kushughulikia athari zinazotokana na uhusiano au
ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(c) utaratibu wa utafutaji na upatikanaji wa mikopo na misaada
kutokana na uhusiano au ushirikano huo;
(d) utaratibu au masharti ya kuvunja au kuimarisha uhusiano au
ushirikiano huo;
(e) utaratibu wa mawasiliano na mashauriano kati ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu
uhusiano au ushirikiano wa kikanda au kimataifa;
(f) utaratibu wa utekelezaji wa masharti ya Ibara hii; na
(g) mambo mengine yatakayohusu uhusiano au ushirikiano wa kikanda
au kimataifa chini ya Ibara hii.

———

Mahusiano kati ya
Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na
Serikali ya Zanzibar

74.-(1) Katika kutekeleza majukumu yake katika maeneo mbalimbali,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itazingatia misingi ya
kushirikiana na kushauriana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la Zanzibar kukuza na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi.
(2) Kwa madhumuni ya kukuza umoja na uhusiano, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, zinaweza
kushauriana na kushirikiana katika mambo yanayohusu uongozi, utawala,
vyombo vya uwakilishi na mahakama.
(3) Utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar au chombo chochote cha Serikali hizo utatekelezwa kwa kuzingatia umoja wa Jamhuri ya Muungano na wajibu wa kukuza utaifa.
(4) Bila kuathiri masharti ya Ibara hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano,
kwa makubaliano maalum baina yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inaweza kutekeleza jambo lolote lililo chini ya mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mujibu wa makubaliano hayo.

———

Wajibu wa
viongozi wakuu
kulinda Muungano

75.-(1) Bila kuathiri wajibu wa kila raia uliotajwa katika Katiba hii, kila
kiongozi mkuu mwenye mamlaka ya utendaji katika Jamhuri ya Muungano
aliyetajwa katika ibara ndogo ya (3) atakuwa na wajibu, katika kutekeleza
madaraka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hii, kuhakikisha kuwa anatetea,
analinda, anaimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(2) Kwa madhumuni ya masharti ya ibara ndogo ya (1) kila kiongozi
mkuu aliyetajwa katika ibara ndogo ya (3), kabla ya kushika madaraka yake, ataapa kuutetea, kuulinda na kuudumisha Muungano kwa mujibu wa Katiba hii.
(3) Viongozi wakuu wanaohusika na masharti ya Ibara hii ni:
(a) Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(b) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
(c) Rais wa Zanzibar;
(d) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano; na
(e) Makamu wa Rais wa Zanzibar.

——–

Utaratibu wa
uchaguzi wa
Rais

86.-(1) Katika uchaguzi wa Rais kila chama cha siasa
kitakachotaka kushiriki katika uchaguzi wa Rais, kitawasilisha kwa Tume
Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria, jina la
mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
(2) Endapo ni mgombea huru, kwa kuzingatia sifa zitakazoainishwa
katika sheria itakayotungwa na Bunge atawasilisha jina lake kwenye Tume Huru ya Uchaguzi.
(3) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais
yatawasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi katika siku na kwa utaratibu
utakaoainishwa katika sheria.
(4) Endapo itafika siku na saa iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu
ambaye anapendekezwa kuwa halali, Tume Huru ya Uchaguzi itawasilisha jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au kumkataa
kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika Katiba hii na sheria.
(5) Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano utafanyika siku
itakayoteuliwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
(6) Mgombea wa nafasi ya madaraka ya Rais atatangazwa kuwa
amechaguliwa kuwa Rais iwapo atapata kura zaidi ya asilimia hamsini ya
kura zote halali zilizopigwa kwa nafasi ya madaraka ya Rais.
(7) Endapo katika uchaguzi wa Rais hakuna mgombea
aliyekidhi masharti ya ibara ndogo ya (6), basi uchaguzi utarudiwa ndani
ya siku sitini kwa wagombea walioshika nafasi ya kwanza na ya pili na
mgombea atakayepata kura zaidi ya asilimia hamsini atatangazwa kuwa
mshindi wa nafasi ya urais.
(8) Mambo mengine yote yahusuyo utaratibu wa uchaguzi wa Rais
yatakuwa kama itakavyofafanuliwa katika sheria itakayotungwa na Bunge kwa ajili hiyo.

———

Madaraka ya
kutunga Sheria

128.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote
yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Bunge.
(2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo
yote yasiyo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi.

(3) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu
jambo lolote katika Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka.
(4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lolote haitatumika
Zanzibar isipokuwa kwa mujibu wa masharti yafuatayo:
(a) Sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na
vilevile Zanzibar au iwe inabadilisha, kurekebisha au kufuta sheria
inayotumika Zanzibar;
(b) Sheria hiyo iwe inabadilisha au kurekebisha au kufuta sheria
iliyokuwa inatumika tangu zamani Tanzania Bara ambayo ilikuwa
inatumika pia Zanzibar kwa mujibu wa Mapatano ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, ya mwaka 1964, au kwa mujibu wa sheria
yoyote ambayo ilitamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na
vilevile Zanzibar; au
(c) Sheria hiyo iwe inahusu Mambo ya Muungano, na kila inapotajwa
Tanzania katika Sheria yoyote ifahamike kuwa sheria hiyo itatumika
katika Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na
masharti ya Ibara hii.
(5) Bila kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba
hii kuhusu mambo yote ya Zanzibar yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba, itakuwa batili.

———

Utaratibu wa
kubadilisha Katiba

129.-(1) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti
yoyote ya Katiba hii kwa kufuata kanuni zifuatazo:
(a) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti ya Katiba hii au
masharti yoyote ya sheria yanayohusu jambo lolote isipokuwa mambo
yanayohusu aya ya (b) au (c), utapitishwa kwa kuungwa mkono kwa
wingi wa kura za Wabunge wote;
(b) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya
Katiba hii au masharti yoyote ya sheria yoyote yanayohusika na jambo
lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika Nyongeza ya Pili, utapitishwa
tu iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge ambao idadi yao
haipungui theluthi mbili ya Wabunge wote wa Tanzania Bara na
theluthi mbili ya Wabunge wote wa Zanzibar;
(c) Muswada wa sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote
yanayohusika na jambo lolote kati ya mambo yaliyotajwa katika
Nyongeza ya Tatu iliyoko mwishoni mwa Katiba hii, utapitishwa tu
iwapo utaungwa mkono kwa zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa
na wananchi wa Tanzania Bara, na zaidi ya nusu ya kura halali
zilizopigwa na wananchi wa Tanzania Zanzibar katika kura ya maoni
itakayoendeshwa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi kwa
mujibu wa sheria.
(2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1)
kubadilisha masharti ya Katiba hii maana yake ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo.

——–

Serikali ya
Mapinduzi ya
Zanzibar na
mamlaka yake

158.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama “Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar” ambayo itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
(2) Bila kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii na katika ibara zifuatazo
katika Sura hii, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaundwa na kutekeleza
madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya 1984.

——

Rais wa Zanzibar
na mamlaka yake

159.-(1) Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Kiongozi Mkuu
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar atakayechaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984.
(2) Rais wa Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya
Jaji Mkuu wa Zanzibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya
Muungano, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar
kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya 1984.

——-

Baraza la
Mapinduzi la
Zanzibar na kazi
Zake

160.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na
wajumbe wa aina na idadi itakayowekwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar ya 1984.

(2) Bila kuathiri madaraka ya Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kama
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Baraza la Mapinduzi litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumsaidia na kumshauri Rais wa Zanzibar katika masuala ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuratibu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia utekelezaji wa madaraka yake juu ya shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu mambo yote yasiyo Mambo ya Muungano,

——-
Baraza la
Wawakilishi la
Zanzibar

161.-(1) Kutakuwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kama
litakavyoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984.
(2) Madaraka yote ya kutunga sheria katika Zanzibar juu ya mambo yote
yasiyo Mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar

——–

Misingi ya
matumizi ya fedha
za umma

243. Misingi ifuatayo itaongoza matumizi ya fedha za umma katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
(a) fedha za umma zitatumika kwa uwazi, umakini na kwa uwajibikaji
pamoja na kuzingatia ushiriki wa wananchi kupitia wawakilishi wao;
(b) mfumo wa fedha za umma utalenga kuwepo kwa:
(i) utozwaji kodi usio wa upendeleo au ubaguzi;
(ii) bajeti ya Serikali inayoweka vipaumbele kwa makundi na
maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo;
(c) matumizi ya rasilimali na mikopo ya Taifa yatazingatia ustawi
linganifu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo; na
(d) taarifa za usimamizi wa fedha za umma zitatolewa katika lugha
inayoeleweka kwa wananchi.

——-

Akaunti ya Fedha
ya Pamoja

244. Serikali ya Jamhuri ya Muungano itatunza akaunti maalum
itakayoitwa “Akaunti ya Fedha ya Pamoja” na ambayo itakuwa ni sehemu ya Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambamo
kutawekwa fedha yote itakayochangwa na Serikali mbili kwa kiasi
kitakachoamuliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha kwa mujibu wa sheria
itakayotungwa na Bunge, kwa madhumuni ya shughuli za Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano.

——-

Tume ya Pamoja
ya Fedha

245.-(1) Kutakuwa na Tume ya Pamoja ya Fedha yenye Wajumbe
wasiozidi saba watakaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa
kushauriana na Rais wa Zanzibar ambapo wajumbe watatu watatoka Zanzibar na wajumbe wanne watatoka Tanzania Bara.
(2) Majukumu ya Tume ya Pamoja ya Fedha yatakuwa ni:
(a) kuchambua mapato na matumizi yanayotokana na, au yanayohusu
utekelezaji wa mambo ya Muungano na kutoa mapendekezo kwa
Serikali zote mbili kuhusu mchango na mgawo wa kila mojawapo ya
Serikali hizo;
(b) kuchunguza kwa wakati wote mfumo wa shughuli za fedha wa
Jamhuri ya Muungano na pia uhusiano katika mambo ya kifedha kati
ya Serikali hizo mbili; na
(c) kutekeleza majukumu mengine ambayo Rais ataipatia Tume au kama
Rais atakavyoagiza, na kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na
Bunge.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara hii, Bunge litatunga sheria itakayoainisha
na kufafanua:
(a) masharti na taratibu za utekelezaji wa majukumu;
(b) masharti kuhusu wajumbe wa Tume;
(c) muundo na majukumu ya Sekretarieti;
(d) taratibu za uwasilishaji wa taarifa za Akaunti ya Pamoja ya Fedha na
taarifa nyingine za Tume kuhusu utekelezaji wa majukumu kwa
mujibu wa Katiba hii; na
(e) mambo mengine yote yanayohusu Tume ya Pamoja ya Fedha.

—–

Mfuko Mkuu wa
Hazina

246. Kutakuwa na Mfuko Mkuu wa Hazina wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano utakaoitwa “Mfuko Mkuu wa Hazina” ambamo fedha zote
zitakazopatikana kwa njia mbalimbali zitawekwa, isipokuwa:
(a) fedha ambazo zimetajwa katika sheria kuwa zitumike kwa
shughuli maalum au ziwekwe katika mfuko mwingine kwa ajili ya
matumizi maalum; au
(b) fedha ambazo kwa mujibu wa sheria, taasisi za Serikali zimeruhusiwa
kukusanya na kubaki nazo kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa taasisi hizo.

——

Masharti ya
kutoa fedha za
matumizi katika
Mfuko Mkuu wa
Hazina

247.-(1) Fedha zinaweza kutolewa kutoka katika Mfuko Mkuu wa
Hazina kwa ajili ya matumizi, kwa kuzingatia masharti yafuatayo:
(a) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa kuwa
yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina na
idhini hiyo iwe imetolewa kwa mujibu wa Katiba hii au sheria; na
(b) fedha hizo ziwe kwa ajili ya matumizi ambayo yameidhinishwa na
sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali itakayotungwa
mahsusi na Bunge au sheria nyingine yoyote iliyotungwa na
Bunge.
(2) Kwa kuzingatia masharti ya ibara ndogo ya (1), fedha zilizomo
katika Mfuko Mkuu wa Hazina zitatolewa kutoka Mfuko huo kwa ajili ya
matumizi kwa kuzingatia masharti kuwa matumizi hayo yawe yameidhinishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
(3) Fedha zilizomo katika mfuko maalum wowote wa Serikali,
isipokuwa Mfuko Mkuu wa Hazina, hazitatolewa kutoka mfuko huo kwa ajili
ya matumizi isipokuwa kwa mujibu wa sheria inayoidhinisha matumizi
hayo.

——

Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya fedha
zilizomo katika
Mfuko Mkuu wa
Hazina

248.-(1)
Rais atatoa maagizo kwa watu wanaohusika watayarishe na
kuwasilisha kwenye Bunge, katika kila mwaka wa fedha wa Serikali, makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kipindi cha mwaka wa fedha wa Serikali unaofuata.
(2) Makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano yaliyotayarishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1), yatawasilishwa kwanza kwenye Kamati husika ya Bunge kwa ajili ya kufanyiwa tathimini na uchambuzi.
(3) Kamati ya Bunge iliyopelekewa makadirio ya mapato na matumizi ya
Serikali kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2), yaweza kukaribisha na kupokea
maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu makadirio hayo, na baada ya kukamilisha tathmini na uchambuzi wa mapato na matumizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kamati itaandaa taarifa yake kuhusu makadirio ya Serikali na kisha kuiwasilisha Bungeni.
(4) Baada ya Bunge kujadili na kuyakubali makadirio ya mapato na
matumizi ya Serikali yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (1),
Serikali itawasilisha kwenye Bunge muswada wa sheria unaohusu matumizi ya fedha ya Serikali, kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina zitakazogharamia shughuli mbalimbali za Serikali zinazohusu makadirio hayo.
(5) Ikiwa katika mwaka wa fedha wowote inaonekana kwamba:
(a) fedha za matumizi zilizoidhinishwa na sheria inayohusu matumizi ya
fedha ya Serikali kwa ajili ya kugharamia shughuli mahsusi hazitoshi;
(b) imekuwa lazima kulipa gharama za shughuli ambayo haikupangiwa
fedha za matumizi kwa mujibu wa sheria za nchi;
(c) kuna fedha ambazo zimetumiwa kwa ajili ya shughuli mahsusi kwa
kiasi kinachozidi kiwango cha matumizi kilichoidhinishwa na sheria
inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali kuhusu shughuli hiyo; au
(d) fedha zimetumiwa kulipia gharama za shughuli ambayo
haikupangiwa fedha za matumizi kwa mujibu wa sheria za nchi,
kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza au, kadri itakavyokuwa, maelezo ya matumizi ya ziada, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio ya matumizi ya nyongeza au maelezo ya matumizi ya ziada, kutawasilishwa kwenye Bunge muswada wa sheria ya matumizi ya fedha ya Serikali au muswada wa sheria unaohusu matumizi ya nyongeza ya fedha ya Serikali kwa ajili ya kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina, na fedha hizo zitagharamia shughuli zinazohusika na makadirio au maelezo hayo.

——-

Utaratibu wa
kuidhinisha
matumizi ya fedha
kabla ya sheria
inayohusu
matumizi ya fedha
ya Serikali kuanza
kutumika

249.-(1) Iwapo mwaka wa fedha wa Serikali umeanza na sheria
inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali inayohusika na mwaka huo
haijaanza kutumika, Rais anaweza kuidhinisha fedha zitolewe kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya kugharamia shughuli za lazima za Serikali, na fedha hizo zitatumiwa ndani ya miezi minne tangu mwanzo wa mwaka wa fedha wa Serikali au hadi sheria inayohusu matumizi ya fedha ya Serikali itakapoanza kutumika, kutegemea ni lipi kati ya mambo hayo litatangulia kutokea.
(2) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya
kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina kwa
kufuata utaratibu ulioelezwa katika ibara ndogo ya (1).

——

Mfuko wa
Matumizi ya
Dharura

250.-(1) Kutakuwa na Mfuko wa Matumizi ya Dharura ambao
matumizi yake yatawekewa masharti katika sheria.
(2) Sheria iliyotajwa katika ibara ndogo ya (1) itaruhusu Rais au
Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha, pale anaporidhika kuwa kuna:
(a) jambo la haraka na la dharura na ambalo halikutazamiwa
kutokea na ambalo halikupangiwa fedha, kuazima fedha kutoka
Mfuko wa Matumizi ya Dharura kwa ajili ya kugharamia jambo hilo;
au
(b) jambo la haraka na la dharura kama ilivyoelezwa katika aya ya (a) ya
ibara ndogo ya (2), kutumia fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya
kugharamia shughuli fulani kulipia gharama za jambo hilo.
(3) Iwapo fedha zimeazimwa kutoka Mfuko wa Matumizi ya
Dharura au fedha zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli fulani
zimetumiwa kugharamia jambo la haraka na la dharura, basi kutawasilishwa kwenye Bunge makadirio ya matumizi ya nyongeza, na baada ya Bunge kuyakubali makadirio hayo muswada wa sheria unaohusu matumizi ya fedha za Serikali utakaowasilishwa kwenye Bunge kwa ajili ya kuidhinisha matumizi hayo utahakikisha kwamba fedha zozote zilizoazimwa kwenye Mfuko wa Matumizi ya Dharura zitarudishwa kwenye Mfuko huo kutoka katika fedha za matumizi yatakayoidhinishwa na muswada huo.

—–

Mishahara ya
baadhi ya
watumishi
kudhaminiwa na
Mfuko Mkuu wa
Hazina

251.-(1) Kutakuwa na watumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambao watalipwa mishahara na posho kama itakavyoelezwa na sheria.
(2) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1), fedha za malipo ya mishahara
na posho za watumishi wa Serikali wanaohusika na masharti ya Ibara hii pamoja na fedha za malipo ya uzeeni na kiinua mgongo, zitatolewa kutoka katika Mfuko Mkuu wa Hazina.
(3) Mshahara anaolipwa mtumishi wa Serikali anayehusika na
masharti ya Ibara hii pamoja na masharti yake ya kazi havitabadilishwa kwa jinsi ambayo itapunguza maslahi ya mtumishi huyo baada ya kuteuliwa, isipokuwa kwamba masharti haya hayahusiki na posho anayolipwa mtumishi huyo.
(4) Endapo mtumishi wa Serikali anayehusika na masharti ya Ibara hii
ana hiyari ya kuchagua kima cha mshahara au aina ya masharti ya kazi, basi kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (3), mshahara wa kima hicho atakaochagua na aina hiyo ya masharti ya kazi atakayochagua vitahesabiwa kuwa vina maslahi zaidi kwake kuliko kima cha mshahara kingine chochote ambacho anaweza kuchagua au aina ya masharti ya kazi nyingine yoyote ambayo angeweza kuchagua.
(5) Masharti ya Ibara hii yatatumika kwa Jaji wa Mahakama ya Juu, Jaji
wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na watumishi wengine watakaoainishwa katika sheria za nchi.

——-

NYONGEZA YA KWANZA
______________
(Imetajwa katika Ibara ya 71(3))
Mambo ya Muungano
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Usalama na usafiri wa anga.
4. Uraia na uhamiaji.
5. Jeshi la Polisi.
6. Sarafu na Benki Kuu.
7. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na Mashirika, ushuru wa forodha na ushuru
wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania na zinazosimamiwa na Idara ya Forodha.
8. Mambo ya nje.
9. Usajili wa vyama vya siasa.
10. Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani.
11. Elimu ya Juu.
12. Baraza la Taifa la Mitihani na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
13. Utabiri wa hali ya hewa.
14. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Maskini yoho yako wewe na ccm wenzako Smz, munaona munawakomoa cuf , kumbe munaidalali Zanzibar na kizazi cha chenu kupoteza kila chao cha Zanzibar.

Share: