Michezo

Kamishna Ali Said apigwa stop kisa kuto kutowajibika ipasavyo

April 7, 2018

Imeandikwa na Salim Hamad , Pemba

Kamati Tendaji ya Chama Cha Soka Zanzibar (ZFA ) taifa Pemba, kimemfungia kamishna Ali Said Ali kwa miezi sita kushika nafasi hiyo kwa kosa la kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.

Akizungumza na mwanamichezo wako Kaimu Msaidizi Katibu wa ZFA taifa Khamisi Hamad Juma alisema Kaminshna huyo alifanya makosa hayo katika mchezo wa Mwenge na Okapi uliopigwa Uwanja wa Gombani wiki iliyopita kwa kuruhusu kuchezwa kwa mchezo huo zikiwa timu zote zimevaa Jezi rangi moja (Nyekundu).

Alisema katika mchezo ya Okapi ilikuja na jezi nyekundu Uwanjani ikiwa kosa lao ni kutokufika kwenye primach metingi wakafanya juhudi ya kubadisha jezi zikiwa jezi hizo ni pungufu wakalazimika kucheza wakiwa wachezaji nane tu uwanjani badala ya kuminamoja.

Hamadi alisema kamati tendaji iliweza kusikitishwa na Kamishna huyo kwa misingi gani aliweza kuruhusu kuchezwa kwa mchezo huo ikiwa yeye ndie aliyepewa jukumu la kusimamia na kufanya kitendo hicho.

Alisema baada ya kuruhusu mchezo huo kuchezwa kilichijitokeza Viongozi wa Okapi walilazimisha kwa nguvu kuingiza wachezaji ambao hawastahiki ndipo muamuzi wa mchezo huo Seif Kesi kuuvunja katika dakika ya 25 ikiwa Mwenge inaongoza kwa mabao 3-0.

‘’Kwa mujibu wa kanuni ya kuendeshea mashindano ya Soka kifungu namba 13 kamishna huyo amesimamishwa kusimamia mchezo kwa kipindi cha miezi sita’’alisema Hamad.

Alisema matokeo ya mchezo huo yalitupiliwa mbali na badala yake Mwenge ilipewa ushindi wa pointi tatu na magoli mawili kwa kufika kwenye primachi ambapo inafanyika siku moja kabla ya mchezo.

Katika hatua nyengine Hamadi alisema kamati tendaji imeitoza faini ya Shilingi laki Nne timu ya Okapi kwa kosa la kuchafua mchezo huo .

Pembatoday

Share: