Michezo

Black Sailors yakata rufaa ZFA

Na Mwajuma Juma

TIMU ya Soka ya Black Sailors imekata rufaa kwa kamati ya Rufaa na Usuluhishi Zanzibar kupinga mamuzi ya ZFA Taifa ya kutaka mchezo kati yao na Viko Pharm urejewe.

Mchezo kati ya timu hizo umepangwa kurejewa leo ambapo Black Sailors imesema kuw haina uwezo wa kugharamia mchezo huo kwa sasa kutokana na muda uliopangwa kuwa mdogo.

Barua hiyo iliyotumwa jana kwa kamati hiyo ilieleza kuwa imeamuwa kutuma lalamiko hilo kwa kamati hiyo ili kuona haki inatendeka baina ya pande mbili hizo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Katibu wa timu hiyo Issa Khatib Masiku imesema kuwa ZFA haikuwatendea haki kwa kukiuka kifungu cha 16 (b) cha kanuni ya mashindano ingawaje katika barua yao walisema kuwa waamuzi na kamisaa walipitikiwa.

“Barua ya ZFA inataka mchezo turejee siku ya Jumamosi (leo), mchezo ambao ulichezwa Jumatano siku ambayo kwa timu yangu haiwezekani kurejea mchezo huo”, alieleza Masiku.

Hata hivyo Masiku kupitia barua hiyo alisema kuwa pamoja na kuwa ZFA imejitetea kwa kusema kuwa imechunguza kw aumakini suala hilo lakini kwa upande wao wamesema kuwa umakini huo haukuwepo kutokana na maamuzi waliyoyatoa.

“Muda ni mdogo ingawaje ZFA inataka ratiba yao isipanguke, sisi hatukujuulishwa mapema kama wenzetu wlaivyofanyiwa, lakini pia timu yangu haikufanyiwa haki kwa kukiukwa kifungu namba 16 (b) cha kanuni ya mashindano”, ilisema Barua hiyo kupitia kw akatibu Masiku.

Hata hivyo barua hiyo ilihoji kuwa pamoja na kuwa waamuzi walipitikiwa je kw aupande wa Viko Pharm na wao ndio walioyafanya hayo kwa kuwadanyanya waamuzi.

Hivyo timu hiyo imeiomba kamati hiyo ya Rufaa na Usuluhishi kutafakari kwa kina suala la mchezo huo ili mwenye haki yake apewe lakini suala la kurudia mchezo siku ya leo ni karibu mno na timu yao haitoweza kufanya hivyo kw asababu ya gharama ya mchezo hawana.

Mchezo kati ya miamba miwili hiyo ulichezwa Machi 14 mwaka huu, huko Fuoni ambapo mwamuzi wa mchezo huo Ramtula Mosi kulivunja pambano hilo baada ya kugunduwa wachezaji wa timu ya Viko Pharm walizidi.

Kitendo hicho kilibainika baada ya mwmauzi huyo kumtoa nje kwa kadi nyekundu mchezaji mmoja wa Viko Pharm na kugundulika wachezaji wakicheza wkaiwa kamili licha ya kutolewa mmoja.

Kwa mujibu wa barua ya ZFA Taifa ya Machi 15 mwaka huu, imetaka mchezo huo kuchezwa leo Machi 17 mwaka huu katika uwnaja wa Mao Dzetung mjini hapa wakati wa saa 10:00 za jioni.

Barua hiyo iliyosainiwa na mjumbe wa ZFA Taifa Masoud Attai ilieleza kuwa ZFA imechunguza kwa makini na kugunduwa kuwa mchezo huo umevunjika kutokana na mwamuzi na kamisaa kjuptikiwa na kutozitekeleza vizuri sheria.

“Kamati Tendaji imekaa kuangalia sababu za mchezo huo kutokumalizika kwa wakati wake kutokana na kuvunjwa na mwamuzi”, alieleza barua hiyo.

Pambano hilo lilivunjika zikiwa zimebakia dakika 7 kumalizika kwa mchezo huo, ambapo tayari Viko Pharm ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0.

Share: