Michezo

Kocha Morocco amuongeza Emanuel Martin Zanzibar Heroes

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemuongeza kwenye kikosi kiungo Mshambuliaji wa timu ya Yanga Emanuel Martin ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA Challenge CUP yanayotarajiwa kuanza Disemba 3-17, 2017.

Katika uteuzi wa awali Martin hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kwenye kikosi cha Heroes kabla ya kubla ya kuchujwa na kubakia 24 ambao wanatarajia kuondoka Zanzibar Jumatano ya Novemba 29.

Martin ambae ni mchezaji wa zamani wa JKU ya Zanzibar ataungana na wenzake Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU), Abdallah Haji “Ninja” (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh “Machupa” (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame “Luiz” (Mlandege), Issa Haidar “Mwalala” (JKU), Abdulla Kheir “Sebo” (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).

Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma “Zimbwe” (Chipukizi), Mohd Issa “Banka” (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman “Pwina” (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim “Seleembe” (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa “Rais” (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

Zanzinews

Share: