Michezo

Timu ya Jamhuri

Na Fatma Said, Zanzibar

WAWAKILISHI wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya Jamhuri wanatarajiwa kuwasili leo visiwani Zanzibar wakitokea Zimbabwe.

Jamhuri ambayo tayari wameshayaaga mashindano hayo baada ya kufungwa mabao 4-1 katika mchezo wao wa marejeano uliochezwa juzi jioni Harare na wapinzani wao timu ya Hwangwe FC.

Kwa mujibu wa Meneja wa timu hiyo Abdallah Elisha msarafa wa timu hiyo wenye wachezaji 18 na viongozi watano ulitarajiwa kuondoka jana mchana na kupitia Ethiopia.

“Msafara wa timu hii utaondoka kesho (jana) mchana kupitia Adi Ababa na kutuwa Zanzibar alfajiri ya leo”, alisema Elisha.

Jamhuri inayaaga mashindano hayo ikiwa imefikisha magoli 7-1 waliyofungwa baada ya mchezo wao wa nyumbani kufungwa mabao 3-0.

Kw aupande wa Tanzania Bara mabingwa wa ligi ya Vodacom timu ya Yanga nayo imeshayaaga mashindano yao baada ya hapo juzi kufungwa ugenini bao 1-0 na Zamalek ya Misri wakati mnyama Simba anaendelea kusonga mbele baada ya juzi kushinda mabao 2-1 dhidi ya Kyovu.

Share: