Michezo

Z’bar Heroes yaingia kambini

Tuesday, 22 May 2012

Sosthenes Nyoni

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar(Zanzibar heroes), Hemed Morocco ametangaza kikosi cha wachezaji 18 watakaoingia kambini leo katika hoteli ya Bwawani tayari ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia la nchi zisizo mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa).

Michuano ya Kombe la Kombe la Dunia la nchi zisizo mwanachama wa Fifa zimepangwa kupigwa nchini Kurdistan kuanzia Juni 4 hadi 9.Akizungumza kwa simu kutoka Zanzibar jana,Msemaji wa Chama cha Soka cha Zanzibar(ZFA)aliwataja wachezaji wanaoingia kambini kuwa ni makipa Abbas Nassoro na Gharib Musa, Ismail Hamis Omari,Mohamed Abdulrahim,Makame Juma na Othaman Omar Tamin.

Wengine ni Amir Hamad,Awadh Juma Issa,Hamis Mcha,Abdulghan Ghulam,Abdulrahim Humod na Abdi Kassim’Babi’.

Pia kuna Juma Othan Mmanga,Selemani Kassim Selembe,Nadir Harpub’Canavaro’,Sabri Ramadhan ‘China’,na Ally Badru.Zacharia alisema kuwa kikosi hicho cha Zanzibar Heroes kitaondoka nchini Juni 2 kuelekea nchini humo tayari kwa kushiriki kombe hilo.”Tunayaomba mashirika,taasisi,makampuni binafsi yatusaidia kwani kuna gharama za kufanikishan kambi ambacho ni kiasi cha Sh 39 milioni,”alisema Zacharia.

Chanzo: Mwananchi

Share: