Mashairi

Mwenzangu..

Mwenza huyu simtaki, yu bado ang’ang’ania,
tena eti kahamaki, , hataki niachilia
Kama vile sina haki, kwa ninacho hitajia
Kajawa na taharuki, haki yangu kuijua

Mwanzo nilimrizia, kwa alivyo nidanganya
Sejua wake uzia, udugu kuuchanganya
sekuwa nikisinzia, hadaze zenikanganya
Hadi kuja nitanzia, alilotaka kufanya

Silaumu wangu baba, ambae kanipeleka
Hakufanya kisiriba, wasia aliuweka
He sema akinikaba, naweza kumuepuka
Ila naona msiba, amezidi kunishika

Ananivuta mashati, kila nikipapatuwa
Kuvuta hewa sipati, nihitajipo pumuwa
Tena ana tashititi, kejeli kajaaliwa
Kaniwekesha shariti, yutayari kuniuwa

By. A. Tajo..

Share: