Burudani

Msanii Kitatange Pemba yunjiani kuihama kampuni yake kisa……

June 12, 2018
Imeandikwa na Salim Hamad, PEMBA

MSANII wa filamu anaefanya kazi zake Kampuni ya Jufe Production kisiwani Pemba, Khatib Omar Khatib “kitatange” amesema yuko mbioni kuikimbia kampuni hiyo, endapo mkataba wake haatorekebishwa, hasa kipengele cha mshahara.

Alisema kwa sasa gharama za maisha zimepanda mara dufu, hivyo kuendelea na mkataba wenye kiwango duni cha mshahara, ni kuendelea kuishi katika maisha ya kubahatisha.

Akizungumza na mtandao huu mjini Wete, msanii huyo alisema, licha ya sanaa yake ya uigizaji, kupokea vizuri na washabiki wake, lakini haoni marekebisho ya mshahara na lakini anaendelea na kuutumikia mkataba mkongwe.

Kitatange, aliejipatia umaarufu mkubwa, kwa wapenzi na mashabiki wake, kwa kule kutumia lugha ya kihindi na kichina, anapokuwa jukwaani, amesema wakati umefika wa uongozi wa Kampuni yake, kuangalia upya suala la mkataba.

“Mkataba nilionao kwa sasa kama vile umeshapitwa na wakati, maana maisha yamepanda lakini mkataba bado, uko vile vile ukiniumiza hasa suala la mapato yangu,”alilalamika.

Alifafanua kuwa iwapo Kampuni hiyo haitobadilika itaweza kuwapoteza wasanii wake wakaenda kujitaftia maslahi sehemu nyengine.

Hata hivyo Kitatange alisema kampuni mpya ya UV Wepesi ambayo inataka kuanzishwa, kama Jufe itashindwa sula kuboresha mkataba huwenda wakajiunga na Kambuni hiyo.

Pia msanii kitatange amewataka wapenzi na washabiki wake kuwa na subra na kuendelea kumuunga mkono katika harakati zake za sanaa.

Pembatoday

Share: