Burudani

UCHAMBUZI WA SANAA ZA BW HAJI GORA HAJI

Zifuatazo ni sanaa za bwana Haji Gora Haji:

1. Ujue Kosa Lako

Hii ni moja kati ya kazi ya kuvutia aliyoitayarisha msanii wetu, Bw Haji Gora. Riwaya hii inaelezea usia uliotolewa na Mzee wa BUSARA kwa mjuu wake anayeitwa MUADILIFU. Mzee wa Busara alikuwa na paka wake aliyejulikana kwa jina la SANURA.

Siku nmoja Mzee wa Busara aliketi mbele ya mjukuu wake, Muadilifu, na kumpa wasia uliosema: “Eee mjukuu wangu; nakupa wasia uuzingatie sana. Kwenye ulimwengu huu usijaribu kutowa kisu penye mkusanyiko wa watu wengi”

Muadilifu aliweza kumiliki kisu kimoja kizuri sana na cha kupendeza. Hali iliyopelekea kila anayekiona kisu kile anavutika nacho. Wako waliofikia hata kutaka kukinunua kwa mamilioni ya Shilingi. Siku moja Muadilifu alipita kwenye eneo na kuwakuta watu wamekusanyika. Alipokwenda kuwauliza alikuta ng’ombe ameanguka na kuvunjika miguu yake miwili ya mbele. Uamuzi ukatoka wa kuwa ng’ombe yule kutokana na hali yake ni bora kuchinjwa. Kati ya wote waliokusanyika pale hakuna hata mmoja alidiriki kumiliki kisu zaidi ya Muadilifu.

Tukikumbuka kuwa Muadilifu ameshapewa wasia na babu yake asichomowe kisu penye kundi la watu. Sikio la kufa halisikii dawa, Muadilifu alichomoa kisu chake kutaka kumuhami ng’ombe yule. Hapo mtoto wa kitajiri ajulikanaye kwa jina la MAJIVUNO alipokiona kisu kilimrusha roho hadi kumwita askari na kumsingizia Muadilifu ameiba kisu chake.

Nini kilimtokea Muadilifu dhidi ya imani yake pamoja na kukiuka wasia wa babu yake. Halkadhalika nini kilimtokezea Majivuno pamoja milki yake aliyokuwa nayo ikichochewa na uchoyo wake, kisa hichi kinaendelea isipokuwa nitamwachia mwandishi amalizie kukulisha ule utamu niliokurambisha.

Hivi ndio hazina yetu hii (Bw Haji Gora) inavyofinyanga sanaa yake. Ni vyema ikiwa kuna mtu miongoni mwetu ambaye yuko tayari kuidhamini sanaa na kuisambaza kila kona ya dunia, asaidie kufanya hivyo.

2. Utenzi wa Paa na Pweza

Hii ndio nyanja Bw Haji Gora anayoogelea – mashairi. Katika utunzi huu msanii wetu anaelezea urafiki wa siku nyingi waliokuwa nao viumbe wawili tofauti, Paa na Pweza. Kama inavyofahamika, Paa ni mnyama anayeishi nchi kavu chakula chake kikuu ni majani. Wakati Pweza ni samaki anayeishi baharini huku chakula chake kikiwa ni majani ya chini ya bahari pamoja na viumbe vyengine vilivyomo baharini.

Mwandishi anasema:

Kisa hichi nakisema
Cha tangu zama na zama
Ni samaki na kinyama
Marafiki walikuwa

Hao ni Paa na Pweza
Urafiki wefanyiza
Na wakuendeleza
Kwa ukaendeleya

Wakati kizungumza
Paa kimwambia Pweza
Ambayo huangamiza
Ajue bila uziya

Alianza kwa kusema
Eee rafiki yangu mwema
Binaadam si mwema
Ukiwaona kimbiya

Viumbe biinaadam
Ndio wetu mahasimu
Maishani mwetu hudumu
Lazima kuwahofia

3. Kisasi

Ni riwaya inayoelezea historia ya paka kwa miaka mingi hadi kufikia kuweka kisasi kuwa popote pale atakapomuona samaki atamla. Kuwa na kisasi hichi ndiko kulikopelekea hadi leo hiii katu paka haingii hata kwenye kidimbwi cha maji. Mwanzoni paka alikuwa anajuwa kuogelea.

4. Utenzi wa Mtoto wa Tumbatu

Kama nilivyotangulia kusema msanii Bw Haji Gora amezamilia zaidi katika sanaa ya mashairi. Utenzi wa Mtoto wa Tumbatu ni miongoni mwa utenzi mrefu kutungwa huku ukikusanya jumla ya beti 483.

Mtoto wa Tumbatu unaelezea kisa kikubwa kilichotokea katika historia ya kisiwa cha Tumbatu. Mnamo mwaka 1945 Tumbatu kisiwani kulitokea moto mkubwa aliosababisha hasara ya nyumba nyingi kuungua kwa moto. Chanzo cha moto huo ni kwa msichana wa kitumbatu kukoka moto wakati wa kupika na kusahau kuuzima. Moto uliweza kuenea na kusambaa sehemu kadhaa za kisiwa hicho. Kama inavyozoweleka kipindi cha kiangazi huku kikisukumwa na upepo wa kaskazi imekuwa chanzo kikubwa cha majanga nchini mwetu hadi leo hii.

Mwandishi anasema;

Ilikuwa msichana Kakwaruza kibiriti
Kapewa kulea mwana Na kukoleza makuti
Ni wakati wa mchana Akazijaza chachati
Ulaji kumpikia Na ndifu akatia

Kaingia mwao ndani Yeye baada kutoka
na chagaa mkononi Moto ukagimbirika
Akaziweka jikoni Macheche kuchachatiuka
Aliyotenda sikia Kiwambani kurukia

5. Kizee Simulizi

Katika riwaya imejumisha hadithi nyingi zenye kuvutia.

6. Maisha ya Haji Gora

Share: